Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

NDANDA FC KUIKABILI YANGA, WATOA NENO KWA MASHABIKI WAO






Leo Jumatano Februari 28, 2018 kutakuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo Ndanda watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani Nangwanda Sijaona kupambana na Yanga kuwania pointi tatu.
Yanga haina historia nzuri inapocheza na Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda-Mtwara. Mechi tatu ambao wamecheza katika uwanja huo hawajawahi kupata ushindi, wamepoteza mchezo mmoja na kutoka sare mara mbili.
Kwa sasa Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 18 pointi nane nyuma ya Simba ambayo inaongoza ligi baada ya kucheza mechi 19.
Yanga imeshinda mfululizo mechi zake tano za VPL za hivi karibuni, ndiyo timu pekee kwenye ligi ambayo imeshinda mechi nyingi katika mechi tano zilizopita. Simba imeshinda mechi nne na kutoka sare mchezo mmoja katika mechi tano zilizopita.
Pamoja na kuwakosa wachezaji wengi kutokana na majeruhi, bado Yanga imeendelea kufanya vizuri kwa kutumia wachezaji wanaopata nafasi ya kuipigania timu yao.
Ndanda ina wachezaji wenye uzoefu wa ligi kama Jacob Masawe, Jabir Azizi Stima, William Lucian, Ame Ally, na kipenzi cha wana Yanga Mrisho Ngasa ambaye alicheza vizuri kwenye mchezo dhidi ya Simba.
Ndanda haiko salama sana, imeshinda michezo mitatu tu msimu huu huku ikiwa imecheza mechi 18 bado wanapambana kuhakikisha wanasalia kwenye ligi kwa ajili ya msimu ujao. Waliwachapa Mbeya City kwa goli 1-0 huko Mbeya na kisha wakaifunga Lipuli Fc kwa goli 2-1 na ushindi wa dhidi ya Stand United kwa goli 1-0.
Ndanda ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 18 (wastani wa kupata pointi moja kwa kila mechi iliyocheza).
Washabiki wa timu ya ndanda FC mkoani mtwara wameombwa kujitokeza kwa wingi kushangilia kwa kujiamini ,kuwatia nguvu wachezaji ili wapate ushindi.
VIDEO:Mwananchi 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top