Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Mwanafunzi Aliyeongoza Kitaifa Matokeo Kidato cha Nne Aahidiwa Ajira Na Benki ya CRDB

Benki  ya  CRDB  imemfungulia  Akaunti  ya  Scholarship  na  kumwekea  sh. Milioni 5  mwanafunzi  aliyefanya  vizuri  katika  mtihani  wa  kumaliza  kidato  cha nne  mwaka  2015,  Butogwa Shija  na  kumwahidi  ajira  pindi  amalizapo  masomo.

Hafla  hiyo  ilifanyika  jana  jijini  Dar  es  Salaam  ikiwa  ni  kuelekea   kilele  cha maadhimisho  ya  siku  ya  wanawake  duniani  leo, ambapo Butogwa  alipewa  zawadi  ili  kuwahamasisha  watoto  wa  kike  kwamba  wanaweza.

Pia  Mamlaka  ya  Elimu Tanzania (TEA)  ilimuongezea  mwanafunzi  huyo  kiasi  cha  shilingi 500,000  lengo  likiwa  ni  kuwahamasisha  watoto  wa  kike  ili  kuleta  haki  sawa  kwa  wote.

Naye Butogwa  aliahidi  kutumia  fursa  hiyo  vizuri  kwa  kusoma  kwa  bidii  bila  kubweteka  na  kuwataka  wanafunzi  wengine  kuweka  bidii  kwenye  masomo  yao.

Katika hatua  nyingine, Naibu Mkurugenzi Mtendaji  wa  CRDB, Esther Kitoka  alisema   wametoa  sh. milioni 20  zitakazosaidia  katika  ujenzi  wa  mabweni  kwa  watoto  wa  kike  ili  kuongeza  kasi ya  ufaulu  kwa  wanafunzi

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA YA CRDB

 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja.
 Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
 Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden
leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka
na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za
wateja
Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa River  lilipo mkoani Arusha  Jenipher Tond akikabidhi zawadi ya tisheti kwa mtoto aliyeshinda kucheza mziki leo sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.

 Watoto wakimkimbiza kuku katika mashindano yaliyofanyika kwenye sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja
 Malindi band ya mkoani kilimanjaro ikitumbuiza sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafanyakazi wa benki pamoja na familia za wateja.
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la USA akikabidhi zawadi kwa mtoto
 Habari picha na Woinde Shizza, Arusha.
BENKI  ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali yachini, kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.

Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani
Arusha  Jenipher Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.

Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.

Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo
imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .
Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaa karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .

“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons.

Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu. 

Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo
zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top