
Huku akiingiza gia kama aonekanavyo dereva huyo ambae jina lake halikupatikana mara anaonekana akiwa kavaa shati lake ambalo ndio sare yake kwa mkono mmoja nao hajapandisha sawasawa kama alivyovaa shati lake.

Dereva akiwa kavaa suruali yake vizuri lakini tatizo ni hilo shati akiwa kaliegesha upande wa mkono wa kulia ili askari wa usalama barabarani akimuona analipandisha juu mabegani ili ''kuzuga'' kama wasemavyo wenyewe vijana wa mjini.Hapo unaona ni tofauti na picha ya mwanzo ambapo shati liko chini mkononi.


Alikuwa makini na kazi yake kama anavyonekana akiangalia upande wa pili(Kulia) kama kuna gari linakuja ili aingie barabarani kutoka kituoni alikokuwa akishusha abiria na kuendelea na safari.Gari hii inafanya safari zake kati ya Tabata Segerea -Tandika. NI Leo asubuhi aliponaswa na kamera ya Rundugai Blog.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Saturday, June 23, 2012
Post a Comment