Mwenyekiti waJumuiya ya Madaktari Tanzania,Dr Steven Ulimboka amesafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.Hatua hiyo imekuja kutokana na pendekezo lililotolewa na jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu kutoa pendekezo hilo kutokana na figo zake kushindwa kufanya kazi vizuri.
Pamoja na usiri mkubwa wakusafirishwa kwake inasemekana amepelekwa nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi.
Katika safari hiyo ameambatana na Kaka yake Dr.Hobakile Ulimboka,Mke wake Dr.Judith Mzovela na Dr.Pascal Lugajo.
Katika hatua nyingine Madaktari walikataa msaada wa Serikali wa Kusadia matibabu yake lakini Madaktari walikata na kuchangishana wenyewe na wananchi walioguswa na hali hiyo hivyo kuweza kupata pesa na kumsafirisha mgonjwa huyo.
Post a Comment