Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Havelange na Teixeira walikula mlungula

Rais wa zamani wa FIFA Havelange

Aliyekuwa Rais wa shirikisho linalotawala mchezo wa soka duniani, FIFA , Joao Havelange pamoja na kiongozi wa soka wakati mmoja nchini Brazil Ricardo Teixeira wanatuhumiwa kupokea mirungura ya mamilioni ya dola za kimarekani kama hongo katika kupanga mwenyeji wa Kombe la Dunia, kwa mujibu wa tangazo la FIFA lililochapishwa jumatano.

Hatimaye shirikisho hilo limechapisha hati ya maelezo kamili kuwa Texeira alipokea faranga za Uswizi milioni 12.74 sawa na dola za Marekani milioni 13 kwa kiwango cha leo kuanzia mwaka 1992 hadi 1997 kama malipo kwa kampuni ya mauzo ya FIFA ikiwa ni mshirika wa ISL. Kufilisika kwa kampuni hiyo yenye makao yake Uswizi kulizusha upelelezi wa kihalifu na kufichua tabia mbovu iliyokuepo ya viongozi kupokea mirungura ili kufanikisha mipango ya wanaohitaji.

Hati hio yenye kurasa 41 ilionyesha kuwa Havelange alipokea malipo ya faranga za Uswizi milioni 1.5 sawa na $milioni moja mnamo mwaka 1997, mwaka mmoja kabla ya kumpisha Sepp Blatter kama Rais mpya.

Ricardo Teixeira

Malipo yanayotajwa kuwa yalipitia benki za raia hao wawili wa Brazil zilifikia kiwango cha faranga milioni 22 za Uswizi kati ya mwaka 1992 na 2000.

Kiwango cha mirungura inayohusiana na hati miliki ya kutangaza Kombe la Dunia pamoja na haki ya kupitisha matangazo wakati wa Kombe la Dunia ilidhihirishwa katika taarifa iliyotayarishwa na mwanasheria wa Wilaya ya Uswizi ya Zug aliyewachunguza Havelange na Texeira kwa matumizi mabaya ya fedha au uongozi usioambatana na misingi ya kazi.

Waraka huu mwanzoni uliwekewa kizuizi usichapishwe tangu Juni mwaka 2010, baada ya wanasheria, FIFA na watu wawili mashuhuri katika Soka duniani kuafikiana juu ya kusimamisha upelelezi wa kihalifu.

FIFA, Havelange na Teixeira walirejesha faranga milioni 5.5 million za Uswizi (takriban dola $6.1 wakati huo) ili mwanasheria Thomas Hildbrand asimamishe uchunguzi na majina yao yawe ni siri.

Teixeira, ambaye alirejesha faranga milioni 2.5, alikanusha madai ya kuhusika kihalifu. Havelange, aliyerudisha laki tano za Uswizi, hakutoa tamko lolote kuhusiana na madai ya uhalifu, kwa mujibu wa taarifa hio.

Chanzo:BBC Swahili.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top