Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KUTOKA BUNGENI:Spika akataa Muongozo wa Mh.Mwigulu Nchemba kuhusiana na Kifo cha Mfuasi wa CCM



KUTOKA BUNGENI:Mh.Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba ameomba muongozo kwa Spika ili bunge lisitishe shughuli zote kwa siku ya Leo ili bunge lijadili kifo cha Mwenyeiti wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),kata ya Ndago Wilaya ya Iramba katika Mkoa wa Singida YOHANA MPINGA(30) alieuawa kwa kupigwa mawe huko Iramba lisitishe huduma za leo bungeni ili wajadili kifo hicho kilichotokea huko Iramba. Anadai kuwa mpango wa mauaji hayo uliandaliwa mapema kwani kuna wabunge ambao walimtumia ujumbe wa maneno kwenye simu yake ya kiganjani ukimtishia kumdhuru yeye na namba za simu amezipeleka Polisi na zinajulikana.

Hata hivyo Spika alimkatisha kwa kumuambia huo sio muongozo kwani alishindwa kusoma vifungu vya kanuni za bunge na pia hatua ya Mh.Mbunge kuanza kutoa Hotuba badala ya kuomba muongozo.Pia akaongeza kuwa jambo hilo linachunguzwa na Polisi ambao watatoa majibu sahihi kuhusu wahusika wa kifo hicho.

Spika aliwaonya waheshimiwa wabunge kuacha mara moja vitendo vya kutishiana pale Mbunge mwenzao anapochangia jambo Bungeni nao wao baadae kutumiana ujumbe wa vitisho.

..........................................
Habari kuhusiana na mauaji hayo bofya na soma
Damu yamwagika Mkutano wa CHADEMA-Habari Leo

Vurugu za Chadema, CCM zaua Singida-Mwananchi

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top