Loading...
Home
» Jamii
» TAARIFA YA SERIKALI KUHUSIANA NA TUHUMA ZA VYOMBO VYA HABARI KUWA MELI ZA IRAN ZINAPEPERUSHA BENDERA TANZANIA
TAARIFA YA SERIKALI KUHUSIANA NA TUHUMA ZA VYOMBO VYA HABARI KUWA MELI ZA IRAN ZINAPEPERUSHA BENDERA TANZANIA
Serikali imepokea taarifa kuhusu tuhuma za meli za Iran kupeperusha bendera za Tanzania ili kukwepa vikwazo
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na SMZ hazitaki kupuuza taarifa hizi. Serikali zote mbili zimeamua kufanya uchunguzi ili kuthibitisha
Tanzania imewaarifu nchi zilizolalamika marafiki kuwaomba kusaidiana nasi kufanya uchunguzi na kushirikiana kuthibitisha taarifa hii
Tumefanya hivyo kwa kuzingatia uwezo wetu wa kiutafiti na kutaka utafiti huu kuwa huru kwa kuwashirikisha wao wenye ujuzi mkubwa
Tunafanya hivyo kwa kuwa wakala wa ZMA anayefanya kazi za kusajili amekana kusajili meli za Iran, Balozi wa Iran nchini aliitwa akakanusha
Tutakapopata matokeo ya utafiti na ikithibitika kuwepo na ukweli hatua zitachukuliwa mara moja
Tukithibitisha tuhuma hizi tutafutilia mbali usajili wa meli hizo
Hatufanyi haya kutokana na barua ya congressman, tunafanya hivyo kutimiza wajibu wetu kimataifa hususan Azimio 1920 la UN Security Council
Tanzani sio adui wa nchi yoyote duniani. Tunafurahia mahusiano yetu na nchi zote duniani
Hili ni jambo linalogusa maslahi ya Tanzania nje na maslahi ya Tanzania ya ndani (Muungano), tujihadhari na namna tunavyolizungumzia
Tusimame pamoja kama taifa. Nchi kwanza!
Chediel . Powered by Blogger.
Post a Comment