Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Taswiraz na Mdau akiwa safarini Kuelekea Moshi


Hapo ni gari zikisogea karibu na mizani ili kupima uzito kama ilivyo kawaida kwa magari makubwa hiyo ni baada ya kuiacha Chalinze.

Ngoma hizo baada ya kupima uzito kwenye mizani na kuponekana hakuna shida yeyote ikianza safari tena huku ikiwa na mzigo wa kutosha hapo.

Ngoma imepaki pembeni baada ya mwendo mrefu inapaki pembeni kwa ajili ya abiria wachimbe dawa ndugu zangu,kama tulivyoikuta pembeni mwa barabara Mabasi yaendayo Arusha yakitokea Dar es Salaamu.

Mambo ya kuchimba dawa hayo! Taratiibu jamaa wanarudi tena ndani ya basi na kuanza kuchapa mwendo.

Kwa mbali kule unaona magari yakishuka kuelekea wami mwendo ukiwa ni taratibu sana kutokana na mteremko ulioko sehemu hiyo.Magari makubwa ya mizigo yakiwa haaswa ndio yanakuwa yanaenda kama yananyata ili kuepusha ajali kutokea.

Hapo unaonekana msafara wa magari zakishuka kwa adamu pale yalipokuwa yanakaribia kushuka/kupita mto wami ambapo hupunguza mwendo hususani yale magari ya mizigo kama unaovyoona kwenye picha.
..........................................................................................................
NI tumaini letu kuwa utakuwa umeguswa kwa namna moja au nyingine kwa taswira na maelezo ya Mdau huyu wa Rundugai Blog aliesafarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top