Mwandishi wetu, Morogoro Yetu
Abiria
mmoja aliyekuwa akisafiri kwa basi la kampuni ya Upendo lililokuwa
likitokea jijini Mbeya kuelekea dar es salaam, amegunduliwa kufariki
dunia ghafla, baada ya basi hilo kufika mjini Morogoro.
Mwili
wa abiria huyo ambaye tiketi aliyokuwa nayo mfukoni imemtambulisha kama
Petro Mrenge Sins, anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Mkoa wa Tabora, umekutwa
umelala katika viti vya chini, nyumba ya basi hilo la abiria, ambapo
baada ya upekuzi, amekutwa akiwa na mfuko wa nailoni maarufu kama rambo
uliokuwa na nguo zake kadhaa, shilingi elfu nne na tiketi ya basi.
Madereva
wa basi hilo la Upendo, Marco Paulo na msaidizi wake Juma Abdul,
wamedai wamegundua kufariki kwa abiria huyo, baada ya kufika, kituo
kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha msamvu mkoani Morogoro, ambapo
walitangaza abiria wanaoshuka wafanye hivyo, lakini hakufanya hivyo na
kuambiwa abiria huyo alionekana kukosa fahamu, ambapo walitoa taarifa
kwa askari waliopo kituoni hapo, na mwili wake kushushwa kituo kikuu cha
polisi cha mjini morogoro.
Abiria
waliokuwa wakisafiri na mzee huyo aliyepoteza maisha, ambaye kiumri
anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 60 hadi 70, tangu majira ya
saa 12 afajiri kutokea mbeya, Josephat Mahaulane na Winfrida Andrew,
wamedai kufahamiana na mzee huyo tangu jumatatu jioni ambapo alisaidiwa
kwa kuchangiwa fedha na wauza matunda wa soko kuu la mjini mbeya na
abiria waliokuwa kituo kikuu cha mabasi, baada ya kudai hakuwa na uwezo
wa kusafiri.
Aidha
wamedai abiria huyo alieleza kutaka kuja mjini Morogoro ambako angeweza
kuonana na ndugu, jamaa na marafiki zake, ambao wangemuwezesha kuelekea
mkoani tabora.
Mwili
wa marehemu huyo ambao pia umekutwa na karatasi ya polisi inayoonesha
alihitaji kusaidiwa kufika Morogoro, umepelekwa kuhifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, ukisubiri
kutambuliwa na taratibu nyingine za kiuchunguzi.
Habari na Morogoro yetu
Post a Comment