Baadhi ya maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu
Kutoka
kushoto ni Meneja Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli,
Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM Mhadhiri wa UDSM,
Dk. Kitila Mkumbo
TAASISI
ya HakiElimu jana jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya
wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau
mbalimbali wa elimu ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Elimu ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla
ya kutoa maoni yao.
Wadau
hao wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya
Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye
mkutano kisha baadaye kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa
kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM,
Dk. Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa
walimu wa juzi pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni
tatizo kwa elimu na kuiingiza kama changamoto.
“Binafsi
kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa
walimu katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara
hiyo…na hata migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa
akijadili katika mkutano huo.
Alisema
wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na
sekondari kwa kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha
tano na sita eneo ambalo limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni.
Alikosoa kiwango cha uwiano kati ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa
kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya walimu wapo shule za mjini huku
hali mbaya ikiwa vijijini.
Aidha
aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo
vikuu ya mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika
bajeti yake. “…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu
imesababishwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa
katika bajeti ya waziri,” alisema msomi huyo.
Kwa
upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM
akizungumza katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya
kawaida hivyo ni vigumu kumaliza changamoto lukuki za elimu
zinazoikabili wizara hiyo.
Alisema
bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa
kuonesha ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa,
bila udhibiti. “…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni
tatizo lingine. Pia uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa
kulinganishwa na waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia
kiwango kinapanda kumbe tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,”
alisema msomi huyo.
Akizungumza
kwenye mjadala Meneja wa Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli
alisema Serikali haiwezi kufanikisha elimu bora bila kuaandaa walimu
bora katika utoaji wa elimu husika. “Huwezi kutegemea elimu bora pasipo
na walimu bora, binafsi sijaona mkakati wowote mahususi wa kuboresha
elimu,” alisema Shuli.
Ameishauri
wizara ya elimu kujiandaa vizuri kimipango kabla ya kutekeleza mpango
wa kuwa na shule ya kidato cha tano na sita kwa kila tarafa ili kuepuka
madudu yaliojitokeza katika mpango wa uanzishwaji shule za kata.
Hata
hivyo kabla ya kuishuhudia bajeti hiyo ikiwasilishwa Dk. Mkumbo na
Mkenda wakiongozwa na mhadhiri mwenzao kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa
Habari na Mawasiliano, Ayoub Rioba waliwasilisha mada zilizokuwa
zikiiangalia elimu ya Tanzania na majaliwa yake.
Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Elimu tayari imewasilisha makadirio ya mapato na
matumizi kwa mwaka 2012/13 ambapo jumla ya sh. 724,471,937,000 ili
zitumike kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu yake. Huku sh.
18,561,689,000 zikiwa ni fedha za ndani na sh. 74,019,627,000 kutoka kwa
washirika wa maendeleo.
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
Post a Comment