Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CHAMA cha Mapinduzi, Wilaya mpya ya Meru, chawaagiza Madiwani kuitisha vikao

CHAMA cha Mapinduzi, CCM, Wilaya mpya ya Meru, kimewaagiza Madiwani wa kata zote katika jimbo hilo la Arumeru mashariki, kuhakikisha wanaitisha vikao vya wanananchi katika kata zao na kusikiliza kero mbalmbali na kuzipatia ufumbuzi na zitakazoshindwa wazipeleke kwenye ngazi za juu .

Hayo yameelezwa jana na Katibu wa Chama cha Mapinduzi,Wiaya mpya ya Kichama ya Meru, Langael Akyoo, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi na wnachama wa CCM,  kwenye ufunguzi wa Tawi jipya la CCM la Nkwamangasha, lililopo kijiji cha Sakila, katika jimbo hilo la Arumeru mashariki.


Akyoo, amewaambia wananchi kuwa tayari Chama cha Mapinduzi kimeshawaandikia Madiwani wote katika Jimbo hilo kuitisha vikao na kuzungumzaia changamoto na kuzipatia ufumbuzi kero zilizopo na Taarifa ipelekwe kwenye Chama kuona utekelezaj wake.


Amesema Madiwani hao lazima wakusanye kero zote katika vijiji vyao hata kama zinawaumiza na kuwakera au wao ndio wahusika wa kukwamisha utatuzi wake na wapeleke taarifa zao katika Chama na kila Diwani awaleze wananchi kuwa amewafanyia nini tangia awe diwani na hiyo ni agenda ya kudumu ya Chama hicho .


Amesema kuwa anatambua zipo kero ambazo hazijatatuliwa sasa umefika wakati  lazima zipatiwe ufumbuzi na kurejesha Imani ya wananchi kwa serikali yao, na Chama katika Wlaya hiyo hakitavumilia kuona kuna baadhi ya madiwani wanashirikiana na watendaji kula fedha za serikali zinaotolewa kwa ajili ya miradi .


" kuanzia sasa Chama kinawatangazia kiyama madiwani na watendaji watakaokula fedha na kukwamisha miradi ".alisema Akyoo.


Akawataka wananchi katika Wilaya hiyo mpya kuunganisha ngvu zao ili kuijenga wilaya hiyo mpya ambayo imezaliwa kutoka wilaya ya Arumeru na kuwataka wananchi wajiepushe na ushabiki wa kisiasa unaochelewesha maendeleo badala yake wafanye kazi kwa maendeleo ya wilaya yao.


Kuhus uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji , utakaofanyika hivi karibuni, Katibu huyo amewataka wananchi na wanachama wa Chama hicho kuhakikisha kinaibuka na viti vyote ukizingatia kuwa katika wilaya hiyo 98%ya wakazi wake ni wanachama wa CCM.


"Katika wilaya yetu hii  hakuna upinzani ila kilichopo ni chuki binafsi ambazo tayari Chama kimeshazipatia ufumbuzi na sasa tunaendelea na mchakat wa kuwarejesha wanachama waliohamia upnzani wakati wa uchaguzi mdogo wa Ubunge,ili tukijenge chama chetu,"alisema Akyoo.


Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kilianzishwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wanyonge hivyo hakiko tayari kuona baadhi ya madwani na watendaji wanakuwa ni kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na CCm, itawatumikia wananchi wote bila kujali itikadi wala dini ya mtu na namna nzuri ya kuwatumikia wananchi ni kuwa na sera nzuri zinazotekelezwa.


Katibu huyo,akawatahadharisha wananchi na wanachama wa CCm,jimboni humo kuepukana na vyama vya kisiasa ambavyo vinafadhiliwa na nchi za nje kwa ajili ya kusambaratisha amani iliyopo nchini  kwa sababu vyama hvyo haviwatakii mema wala amani watanzania.

.

Akaambia wananchi kuwa wanachama wanaohama na kujiunga na vyama vingine wana kasoro hata wakiwafuatlia katika maisha yao watagundua hilo.


Awali Katbu  wa tawi hilo, Victor Yusto Sarakikya, katika  risala, amesema kuwa tawi hilo jipya ambalo limeanzishwa mwaka 2011,lina wanachama hai 117 na lengo ni ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ni kuwa na wanachama hai 300 .


Hivyo akamuomba Chama cha mapnduzi wilayani humo kusaidia kuanzishwa kwa Kijiji kipya ambacho kitazaliwa kutoka kijij cha Sakila ambacho ni kikubwa mno na kinashindwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi.


Amesema tayari wananchi hao wa Nkwamangasha, wapo katika mchakato huo wa kuanzishwa kwa Kijji kpya, li kuharakisha huduma za kijami ikiwezo Zahanati na kuwapunguzia wananchi kusafiri umbali mrefu wa kilometa 7 ,kufuata huduma za matibabu katika Zahanati ya kijij iliyopo Sakila.
Via Full Shangwe 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top