Stephen Kiprotich
........................................................
Mwanariadha wa Uganda ambaye alishinda medali ya
kwanza ya Olimpiki, kwa zaidi ya miaka arubaini iliyopita, amerejea
nyumbani na kulakiwa kwa tahadhima kubwa.
Maelfu ya raia walifurika barabara za mji mkuu Kampala wakati Stephen Kiprotich alipokuwa akielekea katika Ikuli ya rais.Kiprotich, aliandaliwa kiamsha kinywa na rais Yoweri Museveni, ambaye alimkabidhi hundi ya dola elfu themanini za Kimarekani.
Mbali ya zawadi hiyo ya pesa taslim, Kiprotich ambaye alikuwa afisa wa kawaida wa idara ya magereza, sasa amepandishwa cheo na kuwa miongoni mwa maafisa wakuu wa idara ya magereza.
Rais Museveni alitangaza kuwa serikali yake sasa itaanza kuwekaza zaidi katika secta ya michezo.
Kutoka uwanja wa ndege Kiprotich, alisafiri kwa basi maalum iliyoundwa hususan kwa shughuli hiyo yenye nambari ya usajili '' UG GOLD''
Msafara wa Kiprotich ulisimamishwa mara kadhaa na raia ambao walitaka kumuona shujaa wao.
Baada ya kukabidhiwa hundi hiyo Kiprotich, alimuomba rais Museveni kuwajengea wazazi wake nyumba ya kisasa katika maeneo ya Kapchorwa, Kaskazini Mashariki mwa Uganda ombi ambalo lilikubaliwa na rais.
Wakati huo huo rais Museveni, amehaidi kuwa mwanariadha yeyote wa Uganda atakayeshinda medali yoyote katika mashindano ya kimataifa watapokea dola elfu mia nne za Kimarekani.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment