Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini
kabla ya Mahakama kutengua Ubunge wake, Mh Godbless Lema amefungua matawi
katika Kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha juzi August 18,2012.
Katika
ziara hiyo, Lema aliambatana na Mbunge wa Arumeru Masariki Mh Joshua Nassari
pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM kabla ya kujiengua na kujiunga na
Chadema mapema mwezi Aprili mwaka huu, Ndg James Ole Millya, ambao nao kwa
nyakati tofauti walipata fursa ya kuzunumza.
Mbali
na suala la uzinduzi na upokeaji wanachama wapya, Lema alifanya harambee ya
kukusanya fedha kusaidia shughuli za chama hicho katika Kata hiyo ambapo jumla
ya Sh 219,500 zilichangwa na wananchi.
Akiondoka
eneo hilo, Lema alilazimika kuwatuliza mamia ya watu waliokuwa wanafuatilia
msafara wake ili kuepusha kutokea mwanya kwa watu wenye nia mbaya kuleta vurugu
na uharibifu wa mali. Baadae msafara wake ulikatiza mitaa ya Stand Kuu ya mabasi makubwa
na kisha kuelekea bustani ya City Park huku njiani akishangiliwa sana na baadhi
ya watu wakinyoosha vidole kama ishara
ya ushindi.
Huku akiendelea na mikutano hiyo Lema amewasilisha hoja 42 kupinga kuvuliwa Ubunge wake wa Arusha Mjini katika shauri litakalo somwa septemba 20 Mwaka huu.
Lema alivuliwa Ubunge na MAKAHAMA Kuu Kanda ya Arusha, iliyotengua matokeo ya ubunge yaliyompa
ushindi mgombea wa Chadema, Godbless Lema baada ya kuridhika kuwa
alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani
wake katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, Dk Batilda Burian.
Post a Comment