Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Ijue sheria ya takwimu na adhabu yake kwa kukwamisha zoezi la Sensa

SHERIA YA TAKWIMU, SURA 351 (THE STATTISTICS ACR, CAP.351)

1.0 Utangulizi
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Wakala wa Serikali yenye mamlaka ya kisheria ya kutoa takwimu rasmi nchini.

2.0 Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu yameainishwa katika Sheria ya Takwimu, 2002 (Na.1, 2002).

Miongoni mwa majukumu hayo ni kuendelesha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi katika Jamhuri ya Mungano wa Tanzania (To conduct population and Housing Census in the United Republic). Kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Takwimu, 2002.

Aidha, Sheria hiyo inaelekeza kuwa katika kutekeleza majukumu ya kitakwimu ambayo yanaihusisha Tanzania na Zanzibar, NBS itashirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya, Zanzibar (Office oa Chief Gornment Statatician-OCGS). Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.

3.0 Kiapo cha kutunza siri (Oath of secrecy)
Shughuli za NBS ni za kipekee kwa kuwa zinahusu ukusanywaji wa taarifa zinazohusu maisha ya mtu binafsi. Kwa mantiki hiyo, taarifa hizo zinahitaji usiri mkubwa. Katika kudhihirisha jambo hilo, sheria ya Takwimu inaeleza kuwa mtu atakaye husika katika zoezi la ukusanyji wa takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu za Sensa ya Watu na Makazi, atalazimika kuapishwa (kiapo cha kutunza siri) mbele ya Kamishna wa viapo (Commissioner for Oaths) kabla ya kuanza kazi husika. Kifungu cha 11(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002.

4.0 Maofisa walioidhinishwa (authorized Officers)
Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurungenzi Mkuu amepewa mamlaka ya kuwaidhinisha watu wengine kwa lengo kukusanya taarifa maalum za kitakwimu kulingana na mahitaji.

Kifungu cha Sheria ya Takwimu, 2002.

5.0 Amri ya Rais kuhusu kufanyika kwa Sensa ya Watu na Makazi
Sensa ya Watu na Makazi ni shughuli ya kitaifa ambayo katika utekelezaji inahusisha maelekezo ya Rais wa Nchi. Sheria ya Takwimu inaeleza kuwa kabla zoezi la Sensa ya Watu na Makazi halijafanyika, Rais anatakiwa kutoa Amri (Presidential Order) ya kufanyika kwa Sensa. Amri hiyo inatakiwa kueleza:-

a) Tarehe ya kufanyika kwa Sensa;
b) Taarifa zitakazokusanywa katika Sensa;
c) Namna Sensa itakavyofanyika;
d) Muda na mahali Sensa itakapofanyika; na
e) Wahusika katika kukusanya taarifa za Sensa

Kifungu cha 14 cha Sheria ya Takwimu, 2002

6.0 Makosa ya Jinai na Adhabu zake
Sheria ya Takwimu inaainisha vitendo ambavyo ni makosa ya jinai na pia Sheria hiyo inaweka wazi adhabu zinazoweza kutolewa kwa yeyote ambaye atakuwa ametenda makosa hayo.

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takwimu, 2002 kinabainisha makundi ya aina tatu ya watu wanaoweza kushtakiwa kutokana na viten do ambavyo ni makosa kwa mujibu wa Sheria hiyo.

6.1 Waajiriwa wa NBS/ Wadadisi/ Wasimamizi (Authorized Officer)
a. Kutumia taarifa za kitakwimu kwa manufaa binafsi (use of information for personal gain);
b. Kutoa taarifa za kitakwimu bila kibali (publishing any information without authority);
c. Kutoroka/kutelekeza kazi uliyopangiwa kuifanya (desertion);
d. Kudai taarifa tofauti na zilizoruhusiwa kukusanywa (obtaining information not authorized to obtain); na
e. Kuomba malipo/ujira (asking payment or reward).

Vitendo hivyo vyote ujumla ni makosa ya jinai na mhusika akipatikana na hatia atastahili adhabu ya kifungo cha miezi 12 au kulipa faini ya shilingi milioni moja au vyote viwili. Kifungu cha 27(1) a-e) cha Sheria ya Takwimu, 2002.

6.2 Kutoa taarifa zilizopatikana isivyo halali (Mtu yeyote)
Sheria hii inabainisha kuwa ni kosa kwa mtu yeyote kukutwa au kutoa taarifa za kitakwimu zilizopatikana kwa kukika vifungu vya Sheria ya Takwimu. Adhabu kwa makosa ya kundi hili ni kifungo cha miezi 18 au faini ya shilingi milioni moja na laki tano au vyote viwili. Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya Takwimu, 2002

6.3 Kutotoa ushirikiano katika zoezi la kitakwimu (Respondent/ Mtu yeyote)
Sheria hii pia inaainisha makosa yanayowezakufanywa na mtu yeyote au Respondent wakati wa zoezi la kitakwimu (wakati wa kukusanya takwimu). Makosa hayo ni:

a. Kumzuia Authorized Officer (Msimamizi/Mdadisi/Karani wa Sensa kutekeleza majukumu yake)
b. Kukataa /kuacha kwa makusudi:
i. Kujaza fomu au nyaraka yoyote iliyokabidhiwa kwake kwa lengo maalum;
ii. Kujibu maswali aliyoulizwa;

c. Kutoa taarifa za uongo
d. Kuharibu au nyaraka yoyote
e. Kujifanya Authorized Officer kwa lengo la kujipatia taarifa ambazo hastahili kuzipata;
f. Kukataa kutoa nyaraka zozote zinazohitajika katika shughli za kitakwimu;
g. Kukiuka kifungu chochote cha Sheria hii.

Sheria inaeleza kuwa adhabu kwa kosa lolote kati ya hayo ni kifungo cha miezi 6 au faini ya shilingi laki sita. Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya Takwimu, 2002.

7.0 Hitimisho
Sheria ya Takwimu, 2002 imeainisha majukumu ya NBS na kutamka wazi aina za makosa na adhabu zake.

Kwa mantiki hiyo ni kjukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake na kutoa ushirikiano unaostahili katika zoezi la Sensa ya Watu ma Makazi ya Mwaka 2012.

Kwa kufanya hivyo, kila mdau atakuwa ameisaidia Serikali kupata taarifa sahihi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya nchi.

---
Shukurani kwa nukuu ya taarifa hii zimwendee: Elias Mrutu
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top