ALIYEKUWA mwandishi Mwandamizi wa Televisheni ya Channel Ten, Cyprian Musiba (34), amechukuwa fomu
ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa (NEC), na Mkutano
Mkuu wa chama hicho ngazi ya taifa wilayani Bunda mkoani Mara.
Musiba
ambaye amechukua fomu hizo juzi mchana na kuzirudisha jana asubuhi Makao Makuu
ya Ofisi ya CCM Bunda, amesema dhamira yake ya kuomba nafasi hizo mbili ni
kwenda kukijenga chama katika nyanja zote
za
kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Alisema
atapambana kwa nguvu zake zote kudhibiti rushwa, siasa za chuki, fitna na
makundi ndani ya chama chake hicho tawala.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu hizo, Musiba alisema moja
ya mambo yanayokichafua chama chake mbele ya umma wa Watanzania, ni vitendo vya
rushwa, siasa chafu yakiwemo makundi na fitna.
Musiba
alimuomba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Dk.
Edward Hoseah kuwapanga vema makamanda wake kwa ajili ya kuwakamata wagombea na
watu watakaobainika kutoa rushwa ili wachaguliwe kwenye ngwe hiyo ya kuwania
uongozi.
"Nimechukua
fomu hii kwa lengo la kwenda kupigania maendeleo ya
chama
changu tawala. Nitapambana kuhakikisha rushwa, siasa chafu ndani ya CCM
vinaondoka, maana ndiyo vitu vinavyokiharibu kabisa chama.
"Kwa
maana hiyo, kuanzia sasa naiomba TAKUKURU ianze kuwafuatilia na kuwakamata
wagombea wote watakaoonekana kutoa rushwa
wakati
huu wa uchaguzi," alisema Musiba.
Chanzo:Dina Ismail.
Post a Comment