Uhaba wa Viwanja vya Michezo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa watoto wengi kuonyesha vipaji vyao kutokana na kukosa eneo la kuchezea.Ukipita maeneo mengi mijini utakutana na hali hiyo ya ukosefu wa viwanja maalumu kwa ajili ya michezo.
Hili pia limekuwa ni tatizo linalolalamikiwa na wadau wengi kuwa hali hii ndiyo inayorudisha nyuma ukuaji wa Michezo nchini.Hivyo kuwa Taifa linayoshindwa kila mashindano inayoshiriki.Mfano wa karibu ni michezo ya Olimpiki iliyoisha hivi karibuni Nchini Uingereza ambapo Tanzania ilifanya vibaya na kurudi bila medali yeyote.
Kumekuwepo na juhudi za ukuzaji vipaji lakini shida kubwa ni vifaa na viwanja muafaka kwa ajili ya michezo.
Vipi kuhusu sera ya Michezo ya Nchi inasemaje ? Sera hiyo imeshalalamikiwa mno na wadau wa michezo kuwa imepitwa na wakati.
Post a Comment