Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MTATIRO:SEMA "HAPANA" KWA VITA NA MALAWI


SEMA "HAPANA" KWA VITA NA MALAWI.

Mgogoro wa mpaka kwenye ziwa nyasa unaonekana kuchukua sura mpya baada ya kila upande kutamka Uko tayari kwa lolote - maana yake tayari kwa vita.

Sisi kwa Sisi ndani ya nchi tunalilia sana tuwe na amani, Sisi tumekuwa mabingwa wa kupatanisha mataifa mengine, Sisi haohao tuwe mstari wa mbele kuingia vitani! Japokuwa mganga hajigangi lakini afadhali anajua machungu ya kuugua na kukosa dawa na kuchimbiwa kaburi.

Mtizamo wangu ni kuwa, hivi sasa viongozi wa dola yetu wasitunishe misuli kwa majirani zetu, wao wakiongea "nonsense" siye tuwajibu kuwa "meza ya mazungumzo" iamue kila kitu. Tuoneshe ukomavu kama taifa lenye msimamo wa aina yake.

Tutumie kila uwezo wa kiupatanishi kutatua suala hili. Tangu dunia imeanza, vita haikuwahi kuwa na faida hasa kwa wananchi wa kawaida masikini. Pia vita haikuwahi kuwa suluhisho la migogoro, sanasana watu hupigana weeeee na kuuana kwa malaki na mamilioni na bado hukaa mezani kujadiliana, namaanisha baada ya vita hufuata tena majadiliano ambayo yalidharauliwa na kukimbiwa.

Katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, nimeona watu wengi wanashabikia kuwa tusipote muda na ati tuingie vitani kuwakomesha wamalawi, mie siungi mkono. Nasema tukae chini na watu wa Malawi, tutumie kila mbinu na njia za upatanishi na makubaliano, tulimalize suala hili.

Kwa namna yoyote ile tusishabikie vita, nchi iingie vitani pale tu njia zoote za upatanishi zimeshindikana. Kumbukeni kuwa wakati wa vita, bajeti karibu yote ya serikali huishia vitani. Sasa ikiwa tumeingia vitani bila kumaliza njia za usuluhishi tutakuwa tumejiweka kwenye hatari kubwa mno.

Kwa sababu serikali iliyoko madarakani imefanya vibaya kwa miaka 50 sasa, wasipate kisingizio kwa wananchi kuwa miaka ya 2000 hatukupata maendeleo kwa sababu tulikuwa vitani.

Kwenye majukwaa ya 2015 wimbo utakuwa hivi; Mabasi yaendayo kasi hayakupatikana kwa sababu ya vita, barabara za juu hazikujengwa kwa sababu ya vita na Malawi, sera ya matibabu ya wazee haikutekelezeka kwa sababu ya vita na Malawi, kilimo kwanza kilikufa kwa sababu ya vita, mishahara ya wafanyakazi haiongezwi kwa sababu ya vita na Malawi, vijana hawana ajirakwa sababu ya vita........LOL.....

Na kama hatuta-exhorst kwenye mazungumzo ya amani ya muda mrefu, serikali ijipange haraka walete bungeni bajeti mpya ya vita......teh....teh.....teh.....ha ha haaaaa.....(VITA INA TAMU NA CHUNGU ZAKE....WELCOME TO THE WAR).

Haka kabajeti ka-sungura kanakopitishwa dodoma, kasikokidhi mahitaji hata ya mishahara ya walimu, tukaache ka-operate. Mie naamini kuwa suala la mgogoro wa mpaka kati yetu na Malawi litaisha kwa njia za mazungumzo.

Mazungumzo na njia zote za usuluhishi zikishindikana, tuanze kujiandaa na vita, siyo sasa, siyo KABLA ya kukaa mezanu, au siyo tuko mezani tunaongea huku tunatishana.

(Maoni haya yasihusishwe na chama changu na siyo msimamo wa chama), ni maoni yangu binafsi.

Imeandikwa na

Julius Mtatiro.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

3 comments

mie nakupongeza kama hata wewe wa mtaa wa KUGECHA umeliogopa hilo wakati ukurasa wenu ndo tunaoutegemea KIVITA mmh? Basi kwa heshima yako HATUPIGANI NG'O? HUU NI MTIHANI MKUBWA SANA KWA J.M.KIKWETE! NA kwa bahati sana hata mie wa ELIMU ya kawaida nimegundua janja ya nyani coz Huyo mama wa malawi HANA UWEZO WA KIVITA BALI AMETUMIWA NA WAJANJA amerika,Uingereza kwa sababu zao za UROHO wa mali na kumwaga damu za watu wasio na HATIA. HATUPIGANI NG'O? MUNGU ATATUEPUSHA NA LAANA ITAMRUDI MUNGU IBARIKI TANZANIA ,IBARIKI AFRICA AMANI KWETU JADI!!!!!

Reply

hii vita tuiepuke maana hii ni atu wanataka kutuingiza tena kwenye umaskini mwingine teena tumesahau unga wa Yanga jamani

Reply

kazi ipo hapo mabeberu wana taka tu kutugombanisha hawa

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top