WAZIRI
wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa
mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya
wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kauli
hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa
Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana
ucheleweshwaji wa mishahara yao.
Akizungumza
na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam
jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali
kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.
Dk
Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh
bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai
kuanzia leo (jana).
Aliitaja
miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka
viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa
mishahara wafanyakazi hao.
Akizungumzia
madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa
na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa
linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa
pande zote mbili.
Aidha,
alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote
wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.
Katika
hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa
Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha
hizo lilikwishatengwa.
“Nilisikitika
sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha
vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini
hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka”alisema Dk
Mwakyembe.
Awali
Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema
wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote
yanayowakabili wafanyakazi hao.
Alisema
Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali
zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa
mishahara.
Post a Comment