Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Tangazo La Msiba Toronto,Canada

Familia ya Bwana na Bibi Fredrick Kaduma wa Kimara-Dar-es-salaam,Tanzania na watanzania waishio Toronto,Canada wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao, Ritha Kaduma (Fatima) (pichani) kilichotokea juzi tarehe 9th August, 2012 huko Toronto,Canada.Fatuma au Rita amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa kwa muda mfupi.

Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi na kaka yake huko huko Toronto,Canada.

Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki,popote pale ulipo, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika. Gharama zimekadiriwa kufikia kiasi cha $24,000 ambazo zinajumuisha kuutayarisha mwili,kuutunza na kuuhifadhi na pia kuusafirisha mpaka nyumbani Tanzania.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : RBC (Royal Bank of Canada)ACCOUNT NUMBER: 5122551TRANSIT NUMBER: 06742INSTITUTE NUMBER: 003SWIFT CODE: L0YCCAT2

Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwenye anuani pepe gilfa36@hotmail.com .Pia unaweza kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii:

5-7 DRIFTWOOD CRESCENTNORTH YORK,ONTARIO M3N 2R1

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Kaka yake Fatuma (Issa) kwa nambari hii-647-760-1051.

Flora- 647-622-6361Emmanuel -416-835-6778.Gabriel- 416-631-7762.

Kwa upande wa nyumbani Tanzania,tafadhali wasiliana na Fred Kaduma kupitia nambari 0655-888268 kwa taarifa zaidi.

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

- Amen.

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top