Wanafunzi
wa Chuo Kikuu ch Taifa Zanzibar SUZA, wakiwa nje ya Ofisi ya Mhasibu
wa Chuo wakisubiri hatma yao, kuweza kufanya mitihani yao inayotarajiwa
kufanyika wiki ijayo.
Kiongozi
wa Serekali ya Wanafunzi akimuunesha orodha ya Wanafunzi ambao majina
yao yanasubiri malipo yao kutoka Bodi ya Mkopo ya Elimu ya Juu .
Na Mwanajuma Mmanga
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimezuwiya kufanya mitihani
kwa wanafunzi wote ambao hawajakamilisha ada za masomo hali ambayo
imepelekea mgongano na mizozo baina ya wanafunzi na uongozi wa chuo
hicho.
Kauli hiyo imetolewa na wanafunzi wa chuo hicho walipokuwa katika maandamano ya kudai haki yao kufanya mitihani hiyo.
Mmoja
miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho Ali Kombo alisema wiki moja baadae
tunatarajia kufanya mitihani hiyo ghafla wanapokea taarifa ya kuwa kila
mwanafunzi hajakamilisha malipo ya ada hatomruhusu kufanya mtihani
jambo ambalo ni kinyume na matakwa yao.
Pia
alisema kuna baadhi ya wanafunzi wanalipiwa na bodi ya mikopo la taifa
lakini mpaka sasa hawajaingiziwa fedha hizo hali ambayo inarejesha nyuma
masomo yao.
"Sisi
baadhi yetu tushalipiwa na bodi kwa asilimia 90 na kumebaki asilimia 10
tu kwanini wakatuzuilia kutofanya mitihani hiyo. hii fedha kama
asilimia 80 ishalipiwa na bodi wakati hela hiyo inakuja moja kwa moja
inaingia kwenye akaunti" alisema.
Kwa
upande wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Ali Sharifu
Kombo, alisema kuwa yeye binafsi kwa kushirikiana na uongozi wa serikali
yake wameshafuatilia kwenye bodi ya mikopo Tanzania na kuhakikishiwa
kuwa fedha hizo tayari wameshaingiziwa.
Makamu
Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Rai alisema fedha za wanafunzi hao
bado hazijaingizwa nao kama uongozi wanalalamikia kudai ada za masomo ya
wanafunzi kwa lengo la maendeleo ya chuoni hapo.
Sambamba
na hilo Nae Kaimu Meneja wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Patric Show
alisema fedha za wanafunzi hao tayari zimeshaingiziwa katika akaunti zao
na hivyo inawezekana ikawa ni kuchelewa kwa mawasiliano baina ya bodi
na Uongozi wa chuo hicho.
Meneja
huyo wa bodi hiyo alisema mchakato mzima uliosababisha kuchelewa kwa
kufika barua hiyo katika bodi ya mikopo Dar es Salaam kwa muhusika mkuu
ni Sajent wa bodi, lakini kumbe kabla ya hapo Mhasibu wa chuo hicho,
Rukia tayari ameshaingiziwa tokea jana.
Kutokana
na kuchelewa kwa kupelekwa kwa barua hiyo tayari zimeshaingizwa ndani
ya akaunti zao kwa kila mwanafunzi ambae yuko chuoni hapo.
Meneja
huyo amekiri kuwa fedha hizo tayari zimeshaingizwa ndani ya akaunti
hizo jumla ya shilingi milioni 13, kwa orodha ya wanafunzi 58 wa chuo
SUZA.
Hivyo
amewataka wanafunzi hao kuwa wastahamilivu katika kuvuta subra na kuwa
wasikivu kwani mipango yote ishakaa sawa na kila mmoja atapata haki yake
na atafanya mtihani huo.
Post a Comment