INASIKITISHA SANA - VIONGOZI WETU WAMEJERUHIWA VIBAYA ARUSHA
Pamoja na kutoa tahadhari kubwa kwa viongozi wa polisi Arusha, kuwa wenzetu wa CHADEMA wanapanga kwa nguvu zote kuwaogopesha wananchi wa ARusha wasihudhurie mikutano yetu kwa kupanga kuwapiga na kuwaumiza viongozi na wafuasi wetu, jeshi la polisi halikuchukua hatua yoyote.
Hatimaye dkk chache zilizopita, viongozi na wafuasi wetu wamevamiwa na KUPIGWA SANA KWA MAWE na wafuasi wa CHADEMA walioandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Dhahama hii imewakuta viongozi na wafuasi wetu waliotangulia Katika eneo la SOKO LA KILOMBERO kwa ajili ya kuendelea na matangazo ya mkutano wa jumapili.
Mawe yalirushwa kama mvua kuelekea kwa wafuasi wetu bila sababu. Ni marundo ya mawe yaliyokuwa yameandaliwa mahsusi kwa ajili hiyo. Cha kushangaza zaidi ni kuwa HAYA yametendeka mbele ya polisi.
Majeruhi wameshakimbizwa hospitalini.
Tunajua MUNGU yuko kila upande, lakini SIASA za kutafutana kuuana haziwezi kuwasaidia wananchi.
Chama kinawaomba wafuasi wetu mahali popote pale walipo WASILIPIZE KISASI, damu inayomwagwa kimakusudi italipwa kwa mkono wa mungu.
CUF hatutawavizia wanachama na viongozi wa CHADEMA kuwapiga wala kuwaumiza, lakini wakumbuke MALIPO ni hapa hapa.
Chanzo:Julius Mtatiro
Post a Comment