Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA YADUWAZWA NA MTIBWA SUGAR YAKUBALI KIPIGO CHA TATU MTUNGI

 
Watoto wa Jangwani Dar es Salaam Young africans wameendeleza mwanzo mbaya wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 toka kwa wakata miwa Mtibwa Sugar. Matokeo haya ni baada ya kulazimishwa sare tasa na Prison Jijini Mbeya hivyo kuzidi kuwasononesha mashabiki wake walikuwa na shauku ya kupata matokeo mazuri leo hii dhidi ya wakata miwa Mtibwa Sugar lakini kibao kikawageukia na kujikuta wakilala kwa kichapo hicho cha mabao 3-0.

Wakati huo Mnyama ameendelea kuunguruma uwanja wa Taifa baada kui chapa JKT Ruvu 2-0 Kwa mabao ya Amri Kiemba na Haruna Moshi Boban, pamoja na kucheza pungufu baada ya Emmanuel Okwi kupewa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.Hii ikiwa ni mechi ya pili mfululizo mnyama kuzidi kung'ara baada ya kushinda mechi ya ufunguzi wa Ligi hivyo Mnyama kuzidi kuchanua mapema kabisa kileleni pale.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo, Mrisho Ngassa na Emanuel Okwi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top