Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HATIMAYE MARK HUGHES AENDA NA MAJI QPR

MARK HUGHES (kushoto) aliyekuwa Kocha wa QPR ambae ametupiwa virago leo hii baada ya timu kuwa na matokeo mabovu na Kulia ni Harry Redknapp ambae ameteuliwa kuwa Kocha wa QPR .

Baada ya Robert Di Matteo kuonyeshwa mlango wa kutokea leo hii Mmiliki wa QPR Tony Fernandes amempa kisogo Mark Hughes huku timu hiyo ikiwa inajianda na mchezo wake na Manchester United hiyo kesho.

Harry Redknapp ameteuliwa kuchukua nafasi  iliyoachwa wazi na Hughes katika Klabu hiyo yenye makazi Loftus Road.
 
Katika taarifa rasmi ya Klabu hiyo ya QPR ilisema: "Uamuzi huu umechukuliwa kwa uangalifu mkubwa na bodi ya wakurugenzi, kufuatia mikutano iliyofanyika kwa siku kadhaa zilizopita.

"Bodi ya wakurugenzi inamtakia kila la kheri na kumshukuru Mark kwa aliyoifanya katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.

"Mark ameonyesha ueledi na uaminifu katika kipindi chote alichokuwa hapa, lakini kwa hali iliyopo tumejikuta hatuna chaguo zaidi ya kufanya mabadiliko.

"Bodi sasa itafanya kazi kwa nguvu katika kuweka meneja mpya kwa haraka zaidi." 
 
Mark Hughes amekuwa mhanga mwingine wa rungu la wamiliki wa Klabu baada ya kushuhudia Di Matteo akifungashiwa virago(Soma hapa:Di Matteo akutana na rungu la abramovich)
 
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top