Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ISRAEL YARUSHA KOMBORA SYRIA

Wanajeshi wa Israel katika milima ya Golan karibu na mpaka wa Syria
Tukio hilo linakuja wakati makundi ya upinzani ya Syria, yanayokutana Qatar, yametangaza kuwa yametia saini mkataba kimsingi kuwa na shirika moja litalokuwa na serikali ya mpito, na kuwa ndilo linalopokea misaada kwa ajili ya maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji.

Hii ni mara ya kwanza kwa Israil kushambulia jeshi la Syria, tangu vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka wa 1973.

Jeshi la Israil limesema kombora moja lilirushwa dhidi ya Syria, baada ya kituo cha Israil kwenye milima ya Golan kupigwa kwa mzinga.

Hakuna mtu aliyeumia.
Mizinga kadha ya Syria imeshawahi kuangukia upande wa Israil; na waIsraili walisema kuwa watajibu iwapo itatokea tena.

Ni wazi kuwa vita vya Syria vinafurika katika nchi za jirani.
Huku nyuma, upinzani umetangaza kwenye mkutano wao mjini Doha, Qatar, kwamba umekubaliana kimsingi kuunda uongozi wa mseto utaojumuisha makundi yote makubwa yalioko ndani ya Syria na nje.

Mataifa ya magharibi yameahidi kuwa yatatambua na kusaidia ushirika.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top