FT: Swansea 0-0 Liverpool.
Shelvey kidogo aipatie timu yake pointi tatu muhimu kwa shuti lake nje ya18 lakini golikipa anatumai mwili wake kuzuia shuti hilo.
Kemy Agustien akimbadili De Guzman dakika ya 85
Liverpool wamepenya ukuta wa Swansea Sterling na Suarez wakigongeana moja moja lakini shuti la Suarez linatoka nje kwa golikipa Tremmel.
Joe Cole na Jonjo Shelvey wanaingia badala Jordan Henderson na Stewart Downingambao uwepo wao haukuonekana sana
Reina na Dyer wako chini baada ya kugongana na wote wanaonekana wataweza kuendelea na mchezo.
Suarez anashindwa kuiadhibu Swansea baada ya kushindwa kuondoa mpira haraka na matokeo bado Swansea 0 Liverpool 0 (dakika ya 74).
Dyer moja kwa moja anaingia na kupata mpira lakin Downing anazuia na kuwa kona
DK 67:Nathan Dyer anaingia kuchukua nafasi ya Wayne Routledge
Ashley Williams anapiga kichwa na kuokolewa kwenye mstari na Joe Allen
Swansea kupitia Michu wanapata nafasi lakini kichwa chake kinadakwa na Reina. Michu ana magoli mengi ya vichwa(4) kuliko mchezaji yeyote kwenye BPL msimu huu.
Suarez anamlazimisha kipa Tremmel kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira hatari golini
Steven Gerrard anapiga kiki kali na mguu wa kushoto.Ikiwa ni shuti la 10 golini kwa Liverpool lakini linakuwa shuti rahisi kwa kipa Tremmel
DK 8; Hernandez anapata kupiga mpira wa adhabu mita 25 toka lango la Liverpool lakini wanashindwa kutumia nafasi hiyo.
Timu zinatoka kwa ajili ya kuanza kipindi cha Pili.
HALF-TIME Swansea 0-0 Liverpool
Pablo Hernandez bado anakuwa mwiba kwa ukuta wa Liverpool lakini ngoma bado milango ni migumu
DK 34:Sterling ANA PIGA MPIRA UNAGONGA MWAMBA na matokeo bado ni bila kwa bila
Enrique wa Liverpool anatupia kwenye kamba lakini kiungo huyo alikuwa ameotea bado dakika kumi kwenda mapumziko.
Liverpool mara mbili wanapata nafasi lakini shuti la Suarez linazuiwa na Rangel
DK 28;Hakuna goli lakini mpira unavutia kwa timu zote mbili zikishambuliana na kutengeneza nafasi.
DK 25:Swansea 0 Liverpool 0 . Liverpol wameweza kutengeneza nafasi nzuri sana kwa Jose Enrique na Glen Johnson kugongeana lakini kipa anatokea na kuokoa mpira kwenye hatari
DK 22:Hernandez amemfanya Downing wa Liverpool kutokuwa na raha kutokana na umahiri wamchezaji huyo.
Jose Enrique anaingia ndani ya penati box ya Swansea lakini mpira wake unamfikia Luis Suarez ambae anakuwa amezidi nakibendera kiko juu.Enrique angeweza kucheza mpira ule mwenyewe kuliko kutoa pasi.
Pablo Hernandez anakuwa hatari sana upande wa kulia wa Swansea na mpira wake unaondolewa na Skrtel.
DK 15 Bado ngoma ni Swansea 0-0 Liverpool
Dk 11:Liverpool ikiongozwa Suarez wanaingia ndani ya ukuta wa Swans lakini mpira unamkuta Sterling,lakini shuti lake linaenda moja kwa moja kwa golikipa Tremme
DK 8;Chico Flores anajaribu kupiga mpira kutoka mita 35 lakini Agger anazuia mpira huo.
Raheem Sterling (kushoto) na Ben Davies wakipambana kuwania mpira.
KICK-OFF Refa ni Jon Moss anapuliza kipyenga kuanza kwa mechi kati ya Swansea v Liverpool inayochezwa Liberty Stadium
Kocha wa Liverpol Brendan Rodgers ambae anarudi kwa mara ya kwanza Liberty Stadium ambako alikuwa anaifundisha timu ya Swansea kabla ya kuhamia Liverpool.
........
Swansea: Tremmel,
Rangel, Chico, Williams, Davies, Routledge, Britton, Hernandez, De
Guzman, Michu, Shechter
Liverpool: Reina, Skrtel, Agger, Johnson, Enrique, Henderson, Gerrard, Downing, Allen, Sterling, Suarez
Post a Comment