Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowassa akiongea wakati wa Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Kanisa la KKT usharika wa Babati,Mkoa wa Manyara jana.
(Picha na Michuzi Blg)
Ni kuhusu elimu bure hadi sekondari, asema iwe moja ya ajenda za ccm 2015
Kwa ufupi
Lowassa akizungumza jana mjini Babati alisema,
mjadala kuhusu elimu kutolewa bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo
kuwataka wadau wa elimu kuanza sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake
katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Lowassa akizungumza jana mjini Babati alisema,
mjadala kuhusu elimu kutolewa bure hadi sekondari haukwepeki, hivyo
kuwataka wadau wa elimu kuanza sasa kujadili suala hilo na kwamba Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kulifanya hilo kuwa moja ya ajenda zake
katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema elimu ya sekondari ikifanywa bure, itakuwa
ni fursa kwa kila mtoto wa Kitanzania kuipata. Hatua ambayo itaongeza
weledi na uelewa wa mambo mengi katika jamii.
“Ninasema sasa wakati umefika elimu ya sekondari
kuwa kama elimu ya msingi kwa watoto kusoma bure kuanzia kidato cha
kwanza hadi kidato cha nne,” alisisitiza Lowassa ambaye ni Mbunge wa
Monduli (CCM).
Kwa kauli hiyo, Lowassa ni kama ameunga mkono Sera
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao waliingia katika
mgogoro na CCM kuhusu elimu kutolewa bure wakati wa kampeni za Uchaguzi
Mkuu wa 2010.
Chadema wamekuwa wakisisitiza kwamba elimu bure
inawezekana hadi ngazi ya sekondari, lakini wakati wote CCM wamekuwa
wakisema kuwa suala hilo haliwezekani na kwamba kauli za aina hiyo ni
kuwahadaa wananchi.
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, aliyekuwa mgombea wa
urais kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa alitumia sera ya elimu bure
kuanzia chekechea hadi sekondari kama kete ya kusaka ushindi, huku
akisema chama chake kingetenga asilimia 35 ya bajeti kwa ajili ya
kuboresha elimu na kutoa elimu bure.
Hata hivyo, aliyekuwa mgombea wa CCM na baadaye
kupata ushindi, Rais Rais Jakaya Kikwete alikuwa akiwatahadharisha
wapigakura kuwa kwamba ahadi ya Chadema ni hewa na kwamba hilo
lisingewezekana.
Mvutano huo uliwaingiza makada wengine ambao ni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye wakati huo alikuwa Meneja
Kampeni wa CCM na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel
Sitta na kwa upande wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo naye alijitokeza
kutetea sera ya chama chake.
Katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika
Novemba 10, 2010 katika Kata ya Mchangimbore katika Jimbo la Peramiho
mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema “Serikali haiwezi kutoa huduma za
jamii bure” na kwamba lazima wananchi wachangie.
“Nimebahatika kukaa serikalini muda mrefu hiyo
sera ya bure tulijaribu na ikatushinda na wakati huo Hayati Baba wa
Taifa, Mwalimu Nyerere, tulikaa naye tukaona hilo haliwezekani tukaamua
tubadilishe sasa nawashangaa wenzetu wanawadanganya eti watatoa bure.”
Kwa upande wake Dk Slaa akiwa mjini Arusha katika
moja ya mikutano yake alisema kwamba CCM walikuwa wakipinga sera ya
elimu bure hadi sekondari kutokana na kulea ubadhirifu na kuthamini
anasa kuliko maendeleo kwa wananchi.
Kauli ya Lowassa
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga.
Kauli ya Lowassa
Jana akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Babati, Lowassa alisema wakati umefika kwa kila Mtanzania kuzungumzia suala hilo bila ya woga.
"'Ni lazima tukubali na tujadili suala hilo kwa manufaa ya nchi
kwa kila Mtanzania kukubali ushauri huo wa elimu ya sekondari kuwa ya
bure,” alisema Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM) na
kuongeza:
“Tukishakuwa na mjadala wa elimu yetu kuwa bure
hadi ngazi ya sekondari, tena basi iwe ni elimu bora, jambo hili
linapaswa kuwa moja ya ajenda kuu za CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.”
Alisema Serikali inapaswa kugharimia elimu ya
sekondari bila ya woga na kwamba anaunga mkono wito uliotolewa hivi
karibuni na Rais Jakaya Kikwete akiwaagiza watendaji serikalini
kusimamia ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata.
Alisema mafanikio katika ujenzi wa shule za kata
nchini yanatokana na mpango ambao yeye ni mwasisi wake alipokuwa Waziri
Mkuu na kwamba ali aliusimamia kikamilifu kuhakikisha unafanikiwa.
Azungumzia tuhuma
Katika hatua nyingine, Lowassa alizungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba ana utajiri wa kupindukia kwamba siyo za kweli na zinalenga kumpaka matope.
Azungumzia tuhuma
Katika hatua nyingine, Lowassa alizungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba ana utajiri wa kupindukia kwamba siyo za kweli na zinalenga kumpaka matope.
Alisema wale wanaomtuhumu kutokana na yeye
kushiriki katika uchangiaji wa shughuli za kijamii hawamtendei haki
kwani kuchangia siyo kosa.
Lowassa alisema anachokifanya yeye katika shughuli
anayoalikwa huwataarifu marafiki zake kote nchini na kwenda katika eneo
husika na kuchangia na yeye hana utajiri huo kama inavyodaiwa.
Alisema, ataendelea kuchangia bila ya wasiwasi
yeye na marafiki zake na hatishwi na tuhuma hizo kwani siyo za kweli na
aliziita kuwa ni ‘uongo wa kupindukia’.
Naye Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini
Mashariki, Dk Thomas Laizer aliwataka waumini wa kanisa hilo kote nchini
na waumini wa makanisa mengine kuwapuuza baadhi ya watu wenye kutaka
kuleta vurugu nchini.
Askofu Laizer alisema vurugu za kuchoma makanisa
zilizofanyika Mbagala na maeneo mengi zinapaswa zikomeshwe, lakini
akatoa wito kwa waumini Waksrito walioguswa kutokuwa na mawazo ya
ulipizaji wa kisasi.
Alisema, nchini kuna Waislamu wengi wasiounga
mkono vitendo vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya waumini wa dini hiyo,
hivyo makanisa yaombee amani ya nchi, ili Watanzania waendelee kuishi
kwa utulivu.
“Kila mtu mwenye dini afanye maombi kuiombea nchi
amani, yapo makanisa mengi yamechomwa moto na siyo kama waumini wa dini
ya Kikristo ni waoga la hasha, bali mafundisho yetu yanakataza ulipizaji
wa kisasi, kisasi ni kwa ajili ya Mungu,” alisema Askofu Laizer.
Katika harambee hiyo kiasi cha Sh133. 89 milioni
kilichangwa, na kati ya hizo Sh87. 54 ni fedha taslimu na Sh45.85 ni
ahadi. Fedha hizo ni zaidi ya malengo yaliyokuwa yamekusudiwa ya
kuchangisha Sh120 milioni.
Hadi sasa ujenzi wa kanisa hilo umeshagharimu Sh186 milioni na hadi litakapokamilika linatarijiwa kuwa limegharimu kiasi cha Sh600 milioni.
Hadi sasa ujenzi wa kanisa hilo umeshagharimu Sh186 milioni na hadi litakapokamilika linatarijiwa kuwa limegharimu kiasi cha Sh600 milioni.
Chanzo:Mwananchi.
Post a Comment