Manchester United Inaendelea kupunguza deni
................................
Klabu ya soka ya Manchester United imepunguza deni
lake katika robo ya kwanza ya mwaka huu, baada ya familia ya Glazer
inayomiliki timu hiyo, kulipa milioni 62.6.
Kwa jumla, deni lilipungua na kusalia pauni
milioni 359.7, katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe 30 mwezi
Septemba, mwaka 2012.
Deni hilo limepungua kwa asilimia 17, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.
Mapata ya Manchester United yalipanda kwa
asilimia 3.4, na kufikia faida ya pauni milioni 76.3, klabu hiyo ya Old
Trafford imeelezea.
Lakini faida kutokana na utangazaji wa mechi
zake ilipungua kwa asilimia 37.4, na kufikia pauni milioni 13.7, hasa
kutokana na kubadilishwa kwa ratiba za mechi.
Klabu kilicheza mechi moja ya klabu bingwa,
ilhali msimu uliopita ilicheza mechi mbili, na vile vile ilipungukiwa
kwa mechi mbili zilizotangazwa moja kwa moja, ikilinganishwa na msimu wa
awali.
Tofauti hizo zilisababisha hasara ya pauni
milioni 5.6, ilhali klabu kina matumaini kitakuwa katika hali bora zaidi
kwa kucheza mechi zaidi za klabu bingwa.
Manchester United ilipungukiwa kwa milioni 2.6,
kwa kucheza mechi chache za klabu bingwa, hasa kwa kumaliza katika
nafasi ya pili katika ligi kuu ya Premier, msimu 2011-12,
ilikilinganishwa na msimu 2010-11.
Klabu, kwa sasa kinaongoza katika ligi kuu ya Premier.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment