Wananchi
wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara
wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya
uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012
katika kijiji hicho.
Mkazi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bi. Grace
Nyakola (33) akisoma nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano
uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo, leo
alhamisi Nov. 22, 2012.
Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa
ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani
Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22,
2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria
Kashonda na Riziki Ngwali.
Wananchi
wa Kata ya Mliiba Wilayani Tarime mkoani Mara wakisoma nakala za Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na machapisho
mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa
mkutano ulioitishwa na Tume hiyo katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22,
2012
Na Ismail Ngayonga, Tarime, Mara
MKAZI
wa Kata ya Kata ya Mliiba Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo
(31) amependekeza ni vyema Katiba Mpya ikataze vyama vya siasa
vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi wa Rais
visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.
Akitoa maoni yake leo (Alhamisi Nov. 22, 2012)
kuhusu Katiba Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema
kitendo cha kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani
kitaongeza chuki kwa wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa
uchaguzi.
Aidha
Magubo alisema Rais anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya
wananchi wote na hivyo si busara kwa Chama kilichoshida uchaguzi
kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi huyo haongozi wanachama
wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.
“Tazama
Marekani ambao hivi majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika
kampeni za vyama vyao hatukuweza kuona bendera ya Republican wala
Democracy ambavyo vyote vilishiriki uchaguzi na badala yake tuliona
wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na hatukuona bendera ya
Republican wala Democracy” alisema
Alisema
kwa kuwa Tanzania ni nchi ya umoja, amani na mshikamano ni vyema
Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala
ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.
Chanzo:Mara Yetu Blog
Post a Comment