Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (wapili kutoka kulia) akimsikiliza kwa makini
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo, Naiman Mbise alipokuwa akimuelezea matumizi ya
majiko ya kisasa yatakayotumika kufanyia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi Chuo
cha Taifa cha Utalii kilichopo mtaa wa Garden Avenue na Shaaban Robert mkabara
na Chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa na nyumba ya Utamaduni alipotembelea chuo
hicho jana.
Na: Tulizo Kilaga
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ameutaka uongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii
(NCT) kuhakikisha chuo hicho kinatoa elimu yenye ubora wa kimataifa.
Aliyasema hayo Dar es Salaam jana
alipotembelea jengo jipya la Chuo cha Taifa cha Utalii lililopo mtaa wa Garden
Avenue na Shaaban Robert mkabara na Chuo cha IFM na Makumbusho ya Taifa na
nyumba ya Utamaduni kwa mara ya kwanza kuona shughuli zinazofanywa na chuo
hicho.
Mhe. Nyalando alisema chuo hicho
ambacho kina vifaa vya kisasa, kitakuwa na mafanikio zaidi na kutambulika
duniani kote na kuijengea heshima Tanzania iwapo mitaala yake itazingatia zaidi
viwango vya kimataifa.
“Tanzania tunatatizo lakutokuwa
na watu waliobobea katika tasnia ya utalii, kwa chuo hichi cha kisasa hatuna
budi kupanua wigo kwa kuhakikisha mafunzo mengine yanaongezwa bila kusahau
masuala ya lugha za kigeni kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyotambulika
kimataifa na hivyo kuvutia wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi na hata wadau
wa sekta ya utalii nchini kuwapa ajira wahitimu,” alisema Mhe. Nyalando ambaye pia
ni mdau wa sekta ya utalii.
Alisema lengo la Serikali na Wizara
ni kuhakikisha chuo hicho kinakuwa miongoni mwa vyuo bora Barani Afrika chenye
kuzalisha wahitimu wanaotambulika kimataifa. Hivyo kuwa na sifa yakufanya kazi hata
akitoka nje ya mipaka ya nchi.
Waziri Nyalandu alisema Wizara
itahakikisha wakufunzi wa chuo hicho wanapewa nafasi za kwenda kusoma kwenye
vyuo vya nje ili kuongeza ujuzi, kutoa kipaumbele katika mgao wa fedha ili
kukipa uwezo wa kutanua wigo wa mafunzo yake na kukipa uhuru binafsi wa
kiutawala ili suala la ajira liishie kwenye bodi.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo
hicho, Rosada Msoma, alisema chuo hicho kinatoa kozi za miaka miwili kwa ngazi
ya Astashahada na Stashahada na tayari kimeanza na wanafunzi 171 ambao wanajifunza
masuala ya Uzalishaji Chakula, Uokaji, Uandaaji wa Chakula na Vinyaji, Uandaaji
wa Vyumba, Mapokezi, Ugawaji Vyumba na Sanaa ya Mapishi.
Alisema chuo hicho kimejipanga
kuhakikisha wahitimu wake wanakuwa bora katika soko la ajira kwa kuweka
msisitizo kwenye elimu ya nadhalia na vitendo, na tayari chuo kimeanzisha
maeneo ya kitalii yaliopo katika jiji la Dar es Salam kwa ajili ya Safari za
jiji zitakazoongozwa na wanafunzi wanaosoma masomo ya Uongozaji Watalii.
Chanzo:Mjengwa Blog
Post a Comment