Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA:MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AKIKAGUA KIWANJA CHA MAKAO MAKUU YA CHAMA NA UKARABATI WA KUMBI ZA MIKUTANO


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi wengine wakipata maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama juu ya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu na vitega uchumi wa chama hicho mjini Dodoma ambako alisimama kwa muda siku ya Jumanne Novemba 6, 2012
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa ‘White House’ ulio katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kukidhi mahitaji ya sasa. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja. 
Mafundi rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top