 |
Mbunge
wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akihutubia wananchi
waliofurika kwenye uwanja wa Sahara, ambapo pia mbunge huyo alitumia
fursa ya mkutano huo kukabidhi madawati 400 yaliyotengenezwa kwaajili ya
kutatua tatizo la madawati kwa shule za msingi jijini Mwanza. |
Pichani ni baadhi ya madiwani wa
CHADEMA kwa kata mbalimbali jijini Mwanza pamoja na makada wa chama
hicho waliohudhuria kusanyiko hilo kwenye uwanja wa Sahara leo jioni
hapa jijini Mwanza.
Mnamo tarehe 7 mwezi 4 mwaka huu chama
hicho kiliendesha harambee kwenye uwanja huu wa Sahara hivyo madawati
haya ni matokeo ya changizo lililofanyika kwa kishindo kwa wananchi
kujitokeza kuchangia hadi shilingi ya mwisho akibani mwao lakini baadhi
ya wadau wengi na wengine waheshimiwa wabunge wenye majina waliahidi
kwenye mkutano huo wa mwezi wa nne mwaka huu lakini mpaka leo ambapo
tunaelekea kuumaliza mwaka 2012 hawajatimiza ahadi zao licha ya kupigiwa
simu na kufuatiliwa mara kwa mara... Hakika ni maswali kwa wananchi wa
jimbo hili.
 |
Jumla
ya shilingi milioni 56 ikiwa ni ahadi na pesa taslimu zilipatikana
kwenye changizo la madawati lililofanyika mnamo mwezi wa nne 2012 ambapo
pesa cash iliyopatikana ni shilingi milioni 24 ahadi ambayo haijalipwa
mpaka sasa ni shilingi milioni 32. Kujua wanaodaiwa na viwango vya
madeni yao kwa ahadi za madawati |
|
Mbunge
wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akimtambulisha mbunge
wa Ubungo Mh. Peter Mnyika kwa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa
Sahara, ambapo mbunge huyo alitumia fursa ya mkutano huo kukabidhi
madawati 400 yaliyo tengenezwa kwa ajili ya kutatua tatizo la madawati
kwa shule 30 za msingi jijini Mwanza. |
 |
Karibu
na robo ya mwisho wakati Mnyika akielekea kuanza kuhutubia joto la
timbwili timbwili la vurugu likatokea mara baada ya watu kadhaa
waliosadikika kuwa walikuwa wametumwa na maadui wa Wenje ambao wamo
ndani ya chama hicho kufanya vurugu kwenye mkutano huo kwa kurusha mawe
kwenye kusanyiko hali ambayo ilisababisha baadhi ya waungwana
kusambaratika wakihofia usalama wao. |
|
Ili kujinusuru mmoja wa watu hao ilibidi ajisitiri kwenye jukwaa la kuhutubia... |
|
Mdau akitweta mara baada mvua ya makonde kumwangukia.. |
|
Huyu
mwingine alikuwa akilia kwamba wamemfanyia uonevu kumpiga hata
kumuumiza yeye ni mwanachama wa CHADEMA na hajatumwa na mtu. |
|
"Hapa ndipo angalau kuna usalama.." mwananchi akiwa na majeraha yake... |
|
Hatimaye
polisi walifanikiwa kufika eneo la kusanyiko haraka iwezekanavyo na
kuwaondoa watu hao ambao walikuwa wakinyemelewa na wananchi wenye hasira
kali licha ya kukumbilia kwenye jukwaa la viongozi. |
|
Mbunge
wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza Ezekiel Wenje akitoa maelekezo juu
ya madawati hayo ambayo yametengenezwa kwa mtindo kuwa kila moja
linauwezo wa kuketisha wanafunzi watatu.Orodha ya shule zitakazo nufaika na
mpango huo ni pamoja na Shule ya Lake A na B, Shule ya msingi Nyashana
A, B, na C, Shule ya msingi Nyakabungo B, Mabatini A, B na C, Shule ya
msingi Nyerere, Shule ya msingi Mandela, Ngwandu A, B, C na D,
Nyagulugulu, Nyakato, Mahina, Mtakuja, Pamba, Hongera na nyingine ndani
ya wilaya hiyo....
|
 |
Mbunge
wa jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika amelirudia neno lake lililompiga out
Bungeni la kumtaja Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete kuwa ni dhaifu. Akisema kwamba hapa hakuna mwongozo wa
spika, hakuna utaratibu wananchi wamepiga kura....
|
|
Mbunge
Mnyika akikabidhi kiasi cha shilingi laki moja kwa mbunge wa Nyamagana
Ezekiel Wenje kutimiza ahadi aliyoahidi kwenye mkutano uliofayika tarehe
7 mwezi wa 4, 2012 kuchangia madawati kwa shule za msingi wilaya ya
Nyamagana ambapo nyingi ziko katika hali mbaya kwa wanafunzi wake wengi
kuketi chini kwenye vumbi na mawe.Picha kwa Hisani ya G Sengo Blog. | |
Post a Comment