Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

ANGUKO KUU KAMPALA

 
 Wachezaji wa Bara wakijadiliana baada ya kufungwa na Uganda katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge usiku wa leo kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda. Uganda walishinda 3-0 na kutinga fainali, ambako watamenyana na Kenya Jumamosi.Picha na Bongo Staz Blog
.........................  
TANZANIA imepoteza nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Chalenji baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kufungwa na Uganda na Kenya kwenye michezo ya nusu fainali iliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Namboole, Kampala.

Katika mechi hizo, Kili Stars waliondolewa na wenyeji Uganda kwa kichapo cha mabao 3-0, huku ndugu zao Heroes waliondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2 na Kenya baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Uganda walianza kwa kasi na dakika ya sita, Robert Ssentongo alipiga shuti kali lililodakwa kwa ustadi na kipa Juma Kaseja, kabla ya Emmanuel Okwi kuwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika 11 kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ndefu ya Moses Oloya.

 
 Ngassa na John Bocco wakiwa chini ya ulinzi mkali wa beki ya Uganda huku kipa akipangua mpira ili usilete madhara langoni mwake.
Picha na Bongo Staz Blog.
 
Stars waliamka na kuanzisha mashambulizi na dakika 19, mpira wa kichwa wa Erasto Nyoni uligonga besela kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda.

 
 Emanuel Okwi akiwa nje baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Hamisi Kiiza.Okwi ndie mfungaji wa goli la kwanza.Picha na Bongo Staz Blog.
 ................
Uganda walilazimika kufanya mabadiliko mapema baada ya Okwi kutolewa kufuatia kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kiiza.

 
 John Bocco mmoja wa washumbuliaji hatari katika mashindano hayo akijaribu kukokota ngoma katikati ya beki ya Uganda.
Picha na Bongo Staz Blog.
..........
Kiiza alipokea pasi ndefu kutoka upande wa kushoto na kuingia kwa kasi ndani ya eneo la hatari na kupiga krosi iliyounganishwa kwa umakini na Ssentongo dakika 52 na kumaliza ndoto ya Tanzania kusonga mbele.

Ssentongo alifungia Uganda bao la tatu akimalizia mpira uliotemwa na kipa Kaseja dakika 73, lakini dakika 84 taa za uwanja wa Namboole zilizimika na kusababisha mchezo kusimama.

Awali, Zanzibar Heroes mara mbili walipata mabao ya kuongoza, lakini walishindwa kulinda uongozu huo na kujikuta wakilazimishwa sare 2-2 kabla ya kuondolewa kwa mikwaju ya penalti 2-4.

Baada ya sare hiyo, changamoto ya mikwaju ya penalti ilichukua nafasi yake, ambako Heroes ilipata mbili zilizofungwa na Aggrey Morris na Samih Nuhu, huku Khamis Mcha na Issa Othaman wakikosa, wakati Kenya walipata penalti zote nne zilizopigwa na Mike Baraza, Joakins Atudo, Edwin Lavatsa na Abdallah Juma.

Khamis Mcha akishangilia baada ya kuifingia Zanzibar Heroes goli la kwanza katika mechi iliyoamuliwa na changamoto za mikwaju ya penati.Picha na Bongo Staz Blog.
................
Awali, nyota wa Azam, Mcha aliifungia Heroes bao la kwanza dakika 21 akiunganisha vizuri krosi ya Amir Hamad, hata hivyo bao hilo lilidumu kwa dakika nane, kabla ya Kenya kusawazisha baada ya nahodha wa Zanzibar, Nadir Haroub kujifunga wakati akijaribu kukoa mpira mrefu wa juu na kumpita kipa wake Mwadin Ally.

Beki Morris alifungia Heroes bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika 75, baada ya beki wa Kenya, Joakins Atudo kumwangusha ndani ya eneo la hatari Juma Jaku. Hata hivyo, bao hilo lilidumu kwa dakika tano kabla ya Baraza kusawazisha kwa Kenga akiunganisha kwa kichwa kona ya Paul Wene
 
Habari na Mwananchi.
 
Picha na Bongo Staz Blog
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top