Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SIMBA WASAJILI WAKALI WAWILI TOKA THE CRANES

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe (kulia) akiwa Namboole jana kutazama mechi ya Uganda na Tanzania. Baada ya mechi alifanya kazi ya maana kwa klabu yake usiku ambayo anatarajiwa kuimalizia leo.
Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
WEKUNDU wa Msimbazi, wako mbioni kusajili wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, kipa Hamza Muwonge na mshambuliaji Brian Umony, ingawa suala la kocha wa Malawi, Kinnah Phiri halijakaa vizuri bado.
BIN ZUBEIRY jana ilishuhudia mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na mshambuliaji huyo wa zamani wa SuperSport United ya Afrika Kusini kwenye hoteli ya Sheraton mjini hapa.
Hata hivyo, baada ya mazungumzo hayo jana, Simba iliomba mchezaji huyo awasiliane nao leo, ili kwanza watafakari yale anayoyataka.
Kwa ujumla Simba imeridhia kumpa Umony anachokitaka na bila shaka leo watamalizana. Wakati huo huo, Simba inataka kufanya mazungumzo na kipa namba mbili wa Uganda, Hamza Muwonge leo, baada ya kuridhishwa na kazi yake langoni.
Muwonge amekuwa akiidakia Uganda tangu mwanzo wa mashindano haya, alipompokea kipa namba moja, Abbel Dhaira ambaye aliumia kipindi cha kwanza kwenye mechi ya kwanza kabisa ya Kundi A dhidi ya Kenya.
Na katika mechi tano hadi jana alizodaka, kipa huyo hajaruhusu bao hata moja hadi anaipeleka The Cranes fainali, jambo ambalo limewavutia Simba SC na sasa wanaitaka saini yake.
Wakati huo huo, Simba imekosa fursa ya kufanya mazungumzo na kocha wa Malawi, Kinnah Phiri ambaye amerejea kwao na timu yake baada ya kutolewa katika Robo Fainali na Kenya Jumanne.
Simba inamtaka Kinnah baada ya kuona haiwezi kuendelea na kocha wake wa sasa, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick, ambaye kwa sasa yupo kwao Serbia, tangu kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Bara, mwezi uliopita.
Chanzo:Bongo Staz Blog.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top