Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

CCM YAANDAA MPANGO WA KUJITETEA

 Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi
........... 
Kwa ufupi
Akizungumza katika mahojiano ya Kipindi cha Jambo Tanzania yanayorushwa kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi alisema Waziri Mkuu ameagiza mpango huo uanze Desemba 19 mwaka huu.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeandaa mfumo wa utoaji taarifa za utekelezaji wa ahadi zake zilizopo kwenye ilani ya chama hicho, kuanzia mwaka 2005/10, ili kuonyesha hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuzitekeleza.

Hatua hiyo inatokana na agizo la mkutano mkuu wa chama hicho uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma.

Hali kadhalika, agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa wizara zote, mkoa na halmashauri za wilaya kutoa taarifa kupitia vyombo vyote vya habari.

Akizungumza katika mahojiano ya Kipindi cha Jambo Tanzania yanayorushwa kupitia Kituo cha Televisheni cha TBC1, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi alisema Waziri Mkuu ameagiza mpango huo uanze Desemba 19 mwaka huu.

“Wizara zote zitakuwa na vipindi kwenye televisheni kuelezea kwa takwimu, tumetoka wapi na tunakwenda wapi, kila waziri ataeleza hatua tulizofikia kwa sasa, lakini baada ya hapo kila mkoa utakuwa unatoa taarifa za kipindi cha miezi sita halafu wilaya kwa kila kipindi cha miezi minne,”alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema lengo la CCM ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanajenga imani na Serikali yao kupitia ahadi walizopewa wakati wa chaguzi.

“Tunaanza na taarifa za kipindi cha miaka saba kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa, baadaye tutaingia mpaka kwenye utoaji wa taarifa kwa kipindi cha mwezi mmoja katika halmashauri zote,”alisema Lukuvi.

Lukuvi alisema baada ya kutoa taarifa hizo tathimini itafanyika kuangalia idadi na kiwango cha taarifa zilizotolewa kwa wananchi.


Chanzo:Mwananchi
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top