Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

IKULU YATOA ZAWADI KWA WAFANYAKAZI WAKE BORA,YAPOKEA MAKOMBE YA SHIMIWI

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipozi na kikosi kizima cha michezo mbalimbali cha Ikulu Sports Club ambacho kilinyakua jumla ya makombe matano katika michezo mbalimbali ya Shirikisho la Michezo ya Wizara (SHIMIWI) mwaka huu mjini Morogoro. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Deswemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya maka huu mjini Dodoma katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara 56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal, Kuvuta kamba wanawake na wanaume na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha na Bw. Miraji Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa mpigo, akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi akiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha na Bw. Miraji Ahmed Saleh ambaye ameibuka kuwa mfanyakazi Bora na Hodari kwa mpigo, akiwa kama Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi katika Idara ya Huduma za Ikulu na Zahanati katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa wachezaji wa netball wa Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Queens) ya mchezo huo kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa nane toka kulia ) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore (wa pili kushoto ) pamoja na mwenyekiti wa TUGHE tawi la Ikulu Bw. Paulo Mgeni (kulia) wakiwa na Mwadawa Twalibu, Sophie Komba na Pascalia Kibayasa ambao wachezaji wa timu ya netball ya Ikulu Sports Club ambao pia ni wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo huo (Taifa Queens) kwenye hafla ya kuwazawadia iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
PICHA NA IKULU.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top