Kwa maelezo ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
Mh Godbless Lema, vifaa hivyo ni seti kamili pamoja na jenerator kubwa
vinathamani ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 14, pesa ambazo
zilitoka kwa marafiki hao na baadhi ya viongozi wa chama.
Akishukuru
kupatikana kwa vifaa hivyo, Golugwa aliwasifu marafiki hao kwa moyo wa
kujitolea kwa lengo la kusaidia nchi yao, na yeye kuahidi kutoa Sh
milioni moja kusaidia upatikanaji wa gari aina ya FUSO kwa ajili ya
kubebea vifaa hivyo.
Chadema Arusha kupitia Kamati maalulu
waliangaa mjumuiko huo wa marafiki na kuupa jina la “M4C Join The Chain”
ukimaanisha kuwataka wananchi wote wanaokerwa na hali halisi ya mambo
ilivyo wajiunge na harakati za Chadema kisiasa ama kwa kushiriki
kugombea nafasi za uongozi au kusaidia harakati hizo kwa namna
watakavyoweza.
Mjumuiko huo uliwakutanisha marafiki mbalimbali wa
ndani ya Arusha na nje ya Mkoa wakiwemo baadhi ya wafanya biashara
wakubwa Jijini hapa. Chadema Makao makuu waliwakilishwa na Mwenyekiti wa
Chadema Kanda Maalumu ya dar es Salaam, Henry Kileo, huku viongozi
wengi wa Chadema Arusha na madiwani wote wakihudhuria, smbamba na Mh
Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari.
Awali
kulikuwa na hotuba za kutia hamasa kutoka kwa wazungumzaji mbalimbali
walioandaliwa, aliwemo dada yake na Hussein Bashe, Kauthar Mohamed Bashe
aliyewapa ujasiri wanawake kushiriki nafasi za uongozi kisiasa na kuwa
sehemu ya maamuzi katika jamii bila kuwaachia wanaume pekee.
Wazungumzaji
wengine walikuwa ni pamoja na mwanadada aliyejitambulisha kama Aminata
kutoka Korogwe Tanga ambako ana nia ya kuwania Jimbo la Korogwe katika
uchaguzi mkuu ujao, pamoja na Emma Mroso aliyezungumzia tatizo la hofu
miongoni mwa watanzania.
Katika hitimisho lake Katibu huyo alitoa taarifa
ya kusudio la chama chake kuwa na Wiki ya Chadema itakayofikia kilele
siku ya Januari 23, 2013 siku ambayo Chadema itatimiza miaka 20 tangu
kupatiwa usajili wa kudumu kama chama cha siasa nchini.
Akizungumzia
upatikanani wa vifaa hivyo binafsi, Lema alisema kukodisha vifaa ni
gaharama kubwa sana kiasi cha sh laki nne kwa kila mkutano na kudai kuwa
chama hakina uwezo huo na hivyo njia mbadla na nafuu ni kuwa na vifaa
vyao wenyewe. yeye na marafiki zake binafsi aliodai atawatafuta aliahidi
kuchangia milioni 5 katika uchangishaji mwingine kwa ajili ya kupata
gari la matangazo yao ambalo watalitumia kuzunguka maeneo tofauti ya
nchi.
Lema laikumbushia vikwamishi walivyowahi kukutana navyo
katika utaratibu wa awali wa wananchi kuchagia chama chake kwa kutumia
namba 15710 ambapo alieleza kuwako kwa shinikizo toka Serikalini kwa
makampuni ya simu kuwa katika makusanyo yote Chadema wapewe aslimilia 20
tu.
Chanzo:Noise of Silence Blog
Post a Comment