Avram Grant enzi alipokuwa akiifundisha Chelsea kabla ya kufurumushwa akiwa na Rafael Benitez enzi hizo akiwa anaifundisha Liverpool Fc.
Picha na Daily Mail
...........
Chelsea imekanusha madai kuwa kocha wake wa zamani Avram Grant, anarejea tena kumsaidi kocha wa sasa Rafael Benitez.
Benitez hajashinda mechi hata moja tangu aliposajiliwa wiki chache zilizopita, baada ya Roberto Di matteo kufutwa kazi.
Magazetti
kadhaa nchini Uingereza zimeripoti kuwa, Grant ambaye aliongoza Chelsea
hadi fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2008,
atasajiliwa kama mmoja wa washauri wa kiufundi.
''Hakuna ukweli wowote kuhusu madai kuwa Avrant Grant atarejea tena katika klabu ya Chelsea'' alisema msemaji wa klabu hiyo.
Mashabiki wa Chelsea walighadhabishwa sana na
uamuzi wa wasimamizi wa klabu hiyo wa kumfuta kazi Di Matteo na mahala
pake kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Beneitez.
Benitez kwa sasa anakabiliwa na shinikizo chungu
nzima, kufuatia kipigo cha magoli kwa matatu kwa moja walichopewa na
klabu ya West Ham siku ya Jumamosi.
Katika mechi zingine Chelsea ilitoka sare ya kutofungana bao lolote na Manchester Citu na Fulham.
Grant, 57, anaenziwa sana na mmiliki wa klabu
hiyo Roman Abramovich na amekuwa kocha hur tangu alipojiuzulu kama kocha
wa klabu ya Partizan Belgrade mwmezi Mei mwaka huu.
Grant aliongoza Chelsea, kuanzia Septemba mwaka
wa 2007 bada ya Jose Mourinho kuondoka licha ya kuongoza Chelsea
kushinda ligi kuu ya Premier kwa miaka miwili mfululizo, lakini alifutwa
kazi baada ya Chelsea kushindwa kwenye fainali za kombe la mataifa
bingwa barani ulaya na Manchester United kupitia mikwaju ya Penalti.
Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili
Post a Comment