Keki
ilikuwa zawadi nzuri kwa Bi dada Hawa hapo jana.Mungu amjaalie kila
lililo na heri maishani mwake Bi dada Hawa.HAPPY BIRTHDAY Hawaaaa
Wanasema shughuli ni watu na watu wenyewe ndio hao, Khadija mwenye furahaaa teeeleee pale alipomletea zawadi ya Keki Dada yake Hawa nyumbani kwake katika kusherehekea nae siku yake ya kuzaliwa hiyo jana.
Bi dada Hawa mwenye tabasamu teeleee akipozi kwanza kwa picha mbele ya keki inayoashiria umri wake ,,,chezea wewe.
Bi Dada Hawa akilishwa kipande cha keki kutoka kwa mdogo wake Khadija aliyejumuika nae kusherehekea siku yake ya kuzaliwa hiyo jana nyumbani kwake katika sherehe fupi.
Bi dada Hawa akiangalia zawadi kutoka kwa rafikiye Salama ambae alimtumia zawadi kuonyesha uwepo wake katika kumtakia masiha marefu katika siku yake hiyo muhimu ambayo alikuwa nasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Picha kwa Hisani Kubwa ya Mdau Aliyehudhuria Mnuso huo.
Post a Comment