Rais
 wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed 
Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa 
zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya Shahada
 ya Sanaa na Elimu, kwa Sabrina Saidi Rashid,katika sherehe za Mahafali 
ya nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu leo. 
Baadhi
 ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioalikwa 
katika sherehe za Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar 
(SUZA) zilizofanyika leo katika kampasi ya Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja. . 
Wahitimu
 wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ngazi ya Stashahada ya 
Lugha na Elimu, wakati walipokuwa wakitunukiwa na Rais wa Zanzibar na 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) pia Mkuu 
wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),  katika  sherehe za 
mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya 
Tunguu.
Rais
 wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed 
Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ,akitoa 
zawadi kwa mwanafunzi bora katika fani ya Cheti cha Teknolojia ya 
Habari,(IT) kwa Lukuman Mohamed  Bachu,katika sherehe za Mahafali ya 
nane ya Suza,huko katika kampasi ya Tunguu.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 
Post a Comment