Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu. (Picha na Freddy Maro)
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa tatu kushoto), Mama
yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na Sarah Mtweve Dada
yake Ray C
Mwanamuziki wa
Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C amemtembelea Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa
msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema
alifuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve.
Ray C alimweleza Rais kuwa, afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.
Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya
mwanawe na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwa ajili
ya mwanaye waache kufanya hivyo kwa kuwa matibabu ya Ray C yamegharamiwa
na Rais Kikwete.
Post a Comment