Rais wa Rwanda Paul Kagame. Rwanda ina sifa nzuri ya kukaribisha waekezaji wa kigeni.
...............
Watawala nchini Rwanda wametangaza
uamuzi wao kutoa viza kwa waafrika wanaokwenda nchini humo au hata
kupitia huko wakielekea katika nchi zinginezo.
Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi ujao. Sasa nini kimechochea mageuzi haya na kwa nini wakati huu?
Serikali ya Kigali inasema kuwa
hatua hii inalenga kuwafanya watalii zaidi kuingia nchini humo.
Kulingana na idara ya uhamiaji nchini humo, uamuzi huu utasaidia pia
kuondoa tatizo la muda mrefu linaotumiwa na watu wanaoomba viza kutoka
katika mataifa mengi ya Afrika.
Kwa wakati huu,kila mwafrika isipokuwa wale
wanaotoka katika nchi ambazo hazihitaji viza kuingia Rwanda,
watahitajika kujaza fomu hiyo ya kuomba viza kabla ya kuingia Rwanda.
Itawagharimu wasafiri dola thelathini kwa siku
thelathini nchini humo. Ingawa watu wataanza kulipia viza hiyo,kuanzia
Januari mwaka 2013, waafrika wanaosafiri kuelekea Rwanda, wanatahitajika
kupata fumo za viza katika viwanja vya ndege au katika sehemu yoyote ya
mpaka na nchi hiyo.
Msemaji wa idara ya uhamiaji ya Rwanda anasema kuwa hatua hii pia inalenga kuendeleza umoja wa kiafrika kati ya nchi husika.
Rwanda tayari, ina sifa nzuri kimataifa kwa kuwa
nchi nzuri kwa waekezaji. Ingawa nyingi ya pesa inazopata Rwanda
zinatoka kwa nchi za kigeni. Lakini kufuatia uamuzi huo mpya, watawala
wanasema wanalenga kuwavutia wageni kutoka kote barani.
Chanzo:BBC Swahili
Post a Comment