Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

IVORY COAST YAINYOA TUNISIA BILA HURUMA

 Yaya Toure(wa pili kutoka kushoto) akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la pili huku Didier Drogba(kushoto) akijumuika nae.
(Picha na Daily Mail)

 Lacina Traore baada ya kukosa nafasi ya wazi ya kutumbukiza mpira  kwenye kamba katika mechi ambayo Ivory Coast ilishinda kwa mabao 3-0 Tunisia.(Picha na Daily Mail)
Ushindi wa Mabao wa Ivory Coast  3-0 Tunisia katika Uwanja wa   Rustenburg umeisogeza karibu sana na hatua ya nane bora.(Picha na Daily Mail)
 Yaya Toure akijaribu kumzuia Fakhreddine Ben Youssef wa Tunisia katika mpambano ulioishia kwa Ivory Coast 3-0 Tunisia.(Picha na Daily Mail)

 Vimbwanga navyo havikosekani katika mashindano,huyu ni shabiki wa Ivory Coast akiruka kwambwembwe za ainayake katika kukoleza ushindi.
(Picha na Daily Mail)
.................
Ivory Coast inakaribia kufuzu kwa robo fainail ya michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Afrika Kusini katika kundi D.
Ivory Coast imeididimiza Tunisia katika mechi yao ya pili ya kundi D kwa magoli 3-0.
Ivory Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya 21 kupitia kwa nyota wake Gervinho.
Bao la pili limefungwa na Yahya Toure kipindi cha pili dakika ya 85, huku bao la tatu likifungwa na Didier Yakonan katika dakika ya 88.
Tunisia ambayo kipindi cha pili ilionyesha uhai na kufanya mashambulio kadhaa, ilijikuta ikiadhibiwa na wachezaji hao nyota wazoefu wa michuano ya kimataifa.
Matokeo hayo sasa yanamaanisha kuwa Ivory Coast inanukia kufuzu kwa robo fainali ya mashindano hayo.
Ivory Coast itafuzu kwa robo fainali ikiwa itatoka sare ya aina yoyote katika mechi yao ya mwisho na Algeria ambapo itakuwa imezoa alama saba.
Hata hivyo Ivory Coast inaweza kuyaaga mashindano hayo ikiwa Tunisia na Algeria watamaliza kundi hilo na alama sita na kufunga idadi kubwa ya magoli kuliko Ivory Coast.
Kufikia sasa Ivory Coast imefunga magoli matano na kufungwa goli moja.
Ivory Coast sasa ina alama sita, Tunisia nayo inashika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi tatu, huku Algeria na Togo ambazo zitapambana muda mfupi ujao zikiwa hazina pointi baada ya kupoteza mechi zao za kwanza.

HABARI NA BBC SWAHILI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top