Wachezaji wa Yanga wakishangilia katika mechi zilizopita na leo wanatupa karata yao ya kwanza na Prisons ya Mbeya katika Uwanja wa Taifa katika mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
(Picha na Bongo Staz Blog)
NA Chediel.
Young Africans Sports Club Mabingwa wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) leo wanatupa karata yao ya kwanza ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara mzunguko wa PIli pale watakapo toana jasho na Prisons toka Mbeya katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu kutokana na mtani wake wa jadi Simba walioweka kambi Oman kuanza vema mechi yao jana.[SOMA:SIMBA yaipa African Lyon Kipigo] Hivyo na Yanga nao watahakikisha wanshinda mechi yao ili kuweza kuwaonyesha wapenzi wao vitu vya Uturuki[SOMA;YANGA YAANZA MAZOEZI UTURUKI] hivyo mechi hii kuwa na mashamshamu ya kutosha .
Mara baada a kushuka toka Uturuki Yanga ilicheza mechi mbili za kirafiki na Black Leopard kutoka Afrika Kusini katika Uwanja wa Taifa na Kuifunga timu hiyo 3-2 na kurudiana nayo tena Uwanja wa CCM Kirumba na kuitesa tena kwa kuichapa mabao 2-1[SOMA;YANGA YAINYUKA TENA BLACK LEOPARDS MWANZA]
Hivyo Yanga Leo wana kila sababu kuifunga timu ya Prisons ya Mbeya na kuendelea Kujikita kileleni mwa Ligi kuu.
atika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa katika dimba la uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya timu zilitoka sare ya bila kufungana mchezo ambao
pia ulikuwa ni wa waufunguzi katika araundi ya kwanza.
Lakini mpira ni dakika 90 tujumuike ndani ya Uwanja wa Taifa leo milango ya saa 10 jioni kushuhudia vitu vya Ulaya.Nani atatoka kalowa mimi nawe hatujui.

Post a Comment