Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
*Kamati ya Serukamba yaikataa ripoti ya TPA
*Zitto aongoza wabunge kuzibana TBC, TIC
KAMATI ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM) imegoma kuipitia na kuijadili taarifa ya mwenendo na kazi za Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) iliyowasilishwa na Wizara ya Uchukuzi, gazeti la Mtanzania limebaini.
Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya kamati hiyo zinaeleza kwamba, uamuzi wa kukataa kuijadili ripoti hiyo ulikuja baada ya wajumbe wake kuisoma na kubaini kuwapo kwa kasoro kubwa mbili.
Wajumbe kadhaa wa kamati hiyo waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kutotajwa gazetini walisema sababu kubwa ya kwanza iliyosababisha wakatae kuijadili taarifa hiyo ya TPA ni kitendo cha kukosekana kwa ushauri uliotokana na kamati hiyo kwa wizara kuhusu namna ya kuisimamia mamlaka hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, alilieleza gazeti la Mtanzania kwamba, sababu ya pili iliyosababisha walazimike kuirejesha taarifa hiyo ya wizara iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba aliyekuwa ameongozana na Katibu Mkuu wake Omari Chambo ni kubaini kwao kwamba, ilikuwa haijawekwa saini na kiongozi yeyote wa wizara hiyo.
“Tumelazimika kuirudisha taarifa hiyo ya wizara kuhusu TPA baada ya kubaini kasoro kubwa mbili, ya kwanza ikiwa ni ya kutojumuishwa kwa maoni na mapendekezo yetu kwao tuliyoyatoa tuliokutana nao mara ya mwisho na pili ni ya taarifa hiyo kutosainiwa na waziri au kiongozi mwingine yeyote wa wizara. Hili kwetu ni kielelezo cha kasoro na kukosekana kwa uwajibikaji,” alisema mjumbe mmoja wa kamati hiyo.
Mjumbe mwingine aliyezungumza na gazeti hili alisema, sambamba na kuirudisha taarifa hiyo, kamati hiyo ilimwelekeza Tizeba kupeleka ujumbe wao kwao kwa Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe kuhakikisha kwamba yeye mwenyewe anawasilisha taarifa ya wizara yake kuhusu TPA wakati wa mkutano wao ujao ambao umepangwa kufanyika Jumatano wiki ijayo.
Kwa mujibu wa mjumbe huyo, kabla ya hatua ya kuikataa kuijadili kufikiwa, walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa kujua undani wa sakata la kuwasimamisha kazi na lile la kutimuliwa kwa maofisa wengine kadhaa wa TPA akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe.
Mjumbe huyo alimkariri Serukamba akiwaeleza Naibu Waziri na maofisa wa wizara hiyo kwamba, kitendo cha kukosekana kwa maelekezo ya kamati yao katika taarifa ya wizara kilikuwa kikihitaji ufafanuzi ikiwa ni pamoja na kuainishwa sawia.
“Pamoja na kuwepo kwa Naibu Waziri lakini, ripoti ya TPA haijakamilika vizuri na kutokana na hali hii kamati kwa kauli moja tunawarudisha ili mkaiandae vizuri sambamba na kujibu maaagizo ya kamati yaliyatoa kwenu.
“Kwa hali hiyo nendeni mkafanyia marekebisho na mjibu hoja zote mlizoagizwa na kamati katika taarifa yenu na mnatakiwa kurudi hapa Januari 23, mwaka huu ili kuweza kuipitia upya tena ikiwa na marekebisho yanayoeleza kwa kina kuhusu utendaji wenu pamoja na yale yalijiri ,” mjumbe huyo alimkariri Serukamba akiwaeleza wajumbe wa kamati hiyo.
Miongoni mwa mambo ambayo wajumbe wa kamati hiyo waliyataja kuwa miongoni mwa mambo ambayo kamati iliishauri wizara kufuatilia ilikuwa ni pamoja na kuwapo kwa maelezo ya kina kuhusu ujenzi na upanuzi wa gati namba 13 na 14 jambo ambalo linatajwa kuwa moja ya mambo yaliyomng’oa katika wizara hiyo aliyekuwa waziri, Omar Nundu.
“Sisi katika kamati tulihitaji kujua namna upembuzi yakinifu ulivyofanyika kwa kuihusisha kampuni ya kigeni China Communication Construction Company (CCC), kuhusu ujenzi wa gati hizo na kuweka gharama ya dola za Marekani milioni 325.
Jambo jingine ambalo linatajwa kuibua mjadala miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo muda mfupi baada ya kuisoma taarifa hiyo ya wizara ilikuwa ni kukosekana kwa taarifa ya kina iliyokuwa ikieleza kuhusu utendaji wa kazi TPA ambao umesababisha kusimamishwa kazi kwa maofisa wake kadhaa Agosti 23 mwaka jana kabla ya wengine kufukuzwa kazi hivi karibuni.
Chanzo hicho kutoka ndani ya kikao hicho cha kamati kiliiambia MTANZANIA kuwa mbali na hatua hiyo walihitaji kufahamu ripoti ya uchunguzi uliofanywa na kamati iliyoundwa na Waziri Mwakyembe ambayo haikuwamo katika taarifa iliyowasilishwa jana.
Hata hivyo ripoti hiyo ya TPA yenye kurasa 26, iliyowasilishwa mbele ya kamati ya Bunge iligusia masuala machache ikiwemo hali ya utendaji katika kipindi cha mwaka 2007/2012 ambayo ilikuwa ikionyesha kuwapo kwa mafanikio licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.
Katika sehemu moja taarifa ya wizara inaonyesha kwamba, shehena iliyohudumiwa na TPA imeongezeka kutoka tani milioni 11.157 katika kipindi cha mwaka 2010/11 hadi tani milioni 12.084 mwaka 2011/12 ikiwa ni ongezeko la tani 927,000 sawa na asilimia 8.3.
“Mapato na matumizi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yaani mwaka 2007/12 yamekuwa yakiongezeka kwa wastani wa asilimia 26.93 kwa mwaka. Ambapo mwaka 2011/12 TPA ilipata ziada ya Sh milioni 95.3 kutokana na mapato ya Sh milioni 388.99 huku matumizi yakiwa ni Sh milioni 293,650,27,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo ya TPA.
Novemba 6, mwaka jana, Dk. Mwakyembe alitangaza kuivunja Bodi ya Wakurugenzi wa TPA baada ya kufuta uteuzi wa wajumbe wote wa bodi na kisha akateua wajumbe wengine wapya wanane wanaounda bodi hiyo huku mwenyekiti wake akibakia madarakani.
Wakati huo huo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) imeagiza kuanzia Julai mwaka huu, Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) lijiendeshe kwa mapato ya ving’amuzi vya kampuni ya Star Media pekee na kusitisha kutumia matangazo ya biashara.
Pia kamati hiyo, imekitaka Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC), kuondoa msamaha wa leseni iliyotoa kwa kampuni hiyo ya ving’amuzi ikiwa ni pamoja na kuiandikia barua kwa kukiuka masharti ya mkataba kwa kutofikia vigezo vinavyotakiwa.
Agizo hilo lilitolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe Zitto, wakati kamati yake ilipokutana na menejimenti ya TBC na TIC kuhusu mkataba wa huduma za ving’amuzi vya Startimes nchini.
“Tunachotaka shirika hili ni kuwa mali ya umma, watanzania wajibunie nalo kama ilivyo Shirika la Utangazaji wa Uingereza (BBC), hivyo utaratibu huu utaanza Julai mwaka huu, na halitoruhusiwa kuchukua matangazo ili kutoonea mashirika binafsi,” alisema Kabwe.
Kuhusu mkataba wa Starmedia, mwenyekiti huyo alisema kampuni hiyo inamilikiwa na TBC ambayo ina hisa za asilimia 35, kampuni kutoka China asilimia 62 na kampuni ya SDTV ambayo ina hisa tatu na mtaji mzima wa kampuni hiyo kwa mujibu wa TIC ni dola za Marekani milioni 234.
“Hata hivyo, mpaka sasa hakuna hata kampuni moja kati ya hizo iliyokwishatoa fedha za mtaji na fedha zilizowekezwa zinazoendesha huduma ya ving’amuzi ya Startimes ni dola za Marekani milioni 48 chini ya kiwango kilichokubaliwa katika mkataba wake na TIC,” alisema
Alisema kutokana na msamaha huyo TBC ililazimika kulipa dola za Marekani 468,000 sawa na takribani Sh milioni 600 za kitanzania kwa ajili ya leseni hiyo ili kampuni hiyo iweze kutoa huduma.
“Sasa tunaagiza kuanzia sasa fedha hizo zilizolipwa na TBC kwa ajili ya leseni hiyo ndio ziwe mtaji wa TBC kwa kampuni hiyo na kuanzia sasa itakuwa na hisa asilimia 40 badala ya asilimia 35,” alisema Zitto.

CHANZO:MTANZANIA
Post a Comment