Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TAHADHARI YA MVUA KUBWA (KUANZIA 30th Januari - 01 Februari 2013)


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea mvua kubwa yenye ujazo wa zaidi ya milimita 50 kila siku kwa siku zilizotajwa.

Maeneo yanayohisiwa kukumbwa na mvua hizo ni: Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.

Mvua hizo zinatokana na kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo kwa wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavu wanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho
na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi

CHANZO:EATV
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top