Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TCRA YATAKA MCHAKATO WA PUNGUZO LA BEI YA KUPIGA SIMU KATIKA MITANDAO MINGINE UANZE MARA MOJA

 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imeyataka makampuni ya Simu nchini kuhakikisha yanaanza rasmi mchakato wa punguzo la bei ya kupiga simu katika Mitandao mingine, kutoka bei ya Shilingi 113 kwa dakika inayotumika hivi sasa hadi kufikia shilingi 34 na Senti 90.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Profesa JOHN NKOMA, amesema makampuni hayo yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo kuanzia Marchi Mosi mwaka huu, na kubainisha kuwa endapo kampuni yoyote itaonekana kwenda kinyume na maagizo hayo Mamlaka hiyo haitasita kuchukua hatua za Kisheria ikiwa ni pamoja na kufungia leseni ya Biashara ya kampuni hiyo.
 
Aidha Profesa NKOMA amesema kuwa hatua za punguzo hilo zinatokana na kupanda kwa gharama za Maisha miongoni mwa Wananchi, pamoja na kuibuka kwa mtindo wa mtu mmoja kumiliki laini nyingi za Simu kwa lengo la kukwepa gharama kubwa za makato ya kupiga Simu kwenda mtandao mwingine.
 
Kwa upande wao baadhi ya Wananchi waliozungumza, wamesema kuwa Kitendo cha Mamlaka hiyo kuingilia kati suala la kupanda kwa gharama za kupiga Simu kwenye mitandao mingine, kitasaidia kupunguza usunbufu wa muda mrefu uliokuwa ukiwakabili watumiaji wa Mitandao hiyo.
 
CHANZO:CLOUDS FM
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top