Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

JESHI LA POLISI MKOA WA KIPOLISI WA KINONDONI LIMEKANUSHA TAARIFA ZA KUWAUWA MAJAMBAZI

 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni limekanusha taarifa za kuwauwa kwa Majambazi watatu katika eneo la Tegeta usiku wa Kuamkia leo, na badala yake limethibitisha kuuawa kwa Majambazi wawili waliokuwa wakijaribu kufanya tukio la uporaji katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo CHARLES KENYELA, amesema kuwa Majambazi hao wameuawa na Wananchi wenye hasira kali, baada ya kushindwa kufanya tukio la uporaji wa Pikipiki ya mmoja wa wakazi wa eneo hilo, na kubainisha kuwa jeshi hilo kwa sasa linamshikilia mmoja wa majambazi ambaye amenusurika kifo katika tukio hilo.

Katika hatua nyingine Kamanda KENYELA amewataka Wananchi kuwa makini na aina mpya ya ujambazi wa kutumia watoto wadogo,ambao wamekuwa wakipitishwa ndani ya nyumba za makazi kinyemela na kisha kufanya uhalifu, sambamba na kuua mifugo inayotumika kwa ulinzi, ili kutoa nafasi kwa Majamazi wakubwa kuingia ndani kwa urahisi zaidi.

Ifuatayo ni sehemu yak maelezo yak mtoto wa miaka 14 ambaye amekuwa akitumika kwa shughuli mbalimbali za Ujambazi akieleza namna alivyokuwa akitumika.

Wakati huohuo ACP KENYELA ametoa tahadhari ya uwepo wa Magari yasiyo sajiliwa na kujishughulisha na Biashara ya kubeba watu nyakati za usiku, na baada ya hapo watu hao hugeuka na kuwafanyia abiria vitendo visivyofaa ikiwa ni pamoja na uporaji na ubakaji
 
CHANZO:CLOUDS FM
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top