Ni kweli aliyosema Mhe. Rais Mstaafu ndugu Ben Mkapa kwamba harakati za maendeleo hazitakiwi kuwa siri.
Nami nashikilia papo hapo.
Ni kwa nini serikali imeshindwa kuweka wazi mikataba ya bomba la gesi na ujenzi wa nyumba za wanajeshi?
Ninashauri
ndugu zangu Watanzania wote tudai uwazi wa mkataba wa gesi. Achilia
mbali huo wa ujenzi wa nyumba za jeshi. Kwanza tuone huo wa ujenzi wa
bomba la gesi.
Sidai
watuletee wananchi wote tuuone, bali waukabidhi Bungeni kama
walivyoomba Wabunge wapewe hiyo mikataba ipitiwe. Wabunge wameomba tangu
mwaka jana wapewe huo mkataba lakini hadi sasa kumekuwa na kigugumizi.
Sisi tumeshituka kwa kuona serikali imebana kuweka wazi mikataba. Kwani
mikataba ya Tanzania huwekeshwa nje ya nchi kwamba tunapoihitaji atumwe
mtu kuifuata Ulaya au Australia?
Haingii akilini kwamba gharama za ujenzi wa bomba ziko juu kuliko kujenga mtambo wa kusafisha gesi hapo hapo Mtwara.
Ni
kwa nini Watanzania tumewaachia wananchi wa Kusini kulalamika peke yao
bila kuwaunga mkono? Hata nyie wa Uchaggani, Tanga, Uhayani… mtafaidika
tu hata kama gesi itabidi isindikwe huko huko iliko.
Ninashauri tena, Watanzania wote wa ndani na nje ya nchi tudai haki.
Tumechoka
kuibiwa. Ingekuwepo sheria ya kuwataifisha walivyojilimbikizia huenda
na wengine wangeogopa. Baya zaidi, wezi wa kodi zetu hata wakibainika
wanaishia kufukuzwa au kusimamishwa kazi na mabilioni yetu wanaondoka
nayo kuendeleza jeuri mtaani. Maana wanasema kwamba, “hata wakinifukuza
nimeshachota changu nyie mlie tuu,” huo ndio usemi wa mafisadi wa
Kitanzania. Huko tunakoelekea itafika wakati wananchi wenyewe
wanachukuwa hatua ya kugawana mali za mafisadi; Na siyo mbali…
Chanzo - Wavuti
Loading...
Chediel . Powered by Blogger.

Post a Comment