Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA YAANZA MAZOEZI UTURUKI

Wachezaji wa Young Africans wakiwa nje ya hotel ya Fame Residence tayari kwa kuelekea kuanza mazoezi


Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi leo katika Uwanja wa Fame Residence Football - Antalya Uturuki


Kocha wa Magolikipa Razaki Siwa akiwawapa maelekezo magolikipa Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez'
Young Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.

Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameada sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja. 

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top