Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

AFRIKA KUSINI YAAGA FAINALI ZA AFRIKA

 Wachezaji wa Mali wakishangilia kufuzu nusu fainali wakiongozwa Keita
 Wachezaji wa Mali wakiwa wamemzonga golikipa wao baada ya kipenga cha mwisho
 Wachezaji wa Afrika Kusini wakiwa hawaamini macho yao kuwa wametolewa nje ya mashindano baada ya kufungwa na Mali katika mechi iliyoamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
(Picha na Daily Mail)
 Golikipa wa Mali  Soumbeyla Diakite akiokoa mkwaju wa penati wa May Mahlangu wa Afrika Kusini.(Picha na Daily Mail)

Afrika Kusini imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika, baada ya kulazwa magoli matatu kwa moja kupitia mikwaju ya Penalti na Mali.
Timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenziye na hivyo mechi hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kinyume na matarajio ya wengi, wenyeji wa fainali hizo Afrika Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupiga mikwaju yake na kufanikiwa kupata mkwaju wa kwanza pekee.
Mali ilijibu kwa kufunga mikwaju mitatu na katika mkwaju wa kuamua ikiwa wataendelea, mkwaju uliopigwa na mchezaji wa Afrika kusini ulipaa juu ya goli na hivyo kuwapa Mali ushindi bila kupiga mkwaju zaidi.
Mali na Ghana tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wengine wawili kuamuliwa katika mechi baina ya Nigeria na Ivory Coast na Togo na Burkina Faso siku ya Jumapili.
Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.
Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.

CHANZO:BBC SWAHILI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top